Askari polisi na wasamaria wema
wakisaidia kutoa maiti kutoka katika basi la Lupondije Express namba T
798 AKV kutoka Mwanza - Iringa baada ya kupinduka eneo la Mteremko wa
Ipogolo mjini Iringa.
NA RAYMOND MINJA IRINGA
Watu sita wamefariki dunia na wengine zaidi ya 38 kujeruhiwa na kulazwa kwenye hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Mwanza kwenda Iringa kupinduka kwenye mlima Ipogolo uliopo Manispaa ya Iringa.
Mganga mkuu wa mkoa wa Iringa Robert Salim alisema waliokufa kwenye ajali hiyo ni sita ambapo wawili kati ya hao walifariki wakiendelea kupata matibabu kwenye hospitali hiyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba alisema ajali hiyo ilitokea jana (juzi) saa 3:30 usiku baada ya basi la Lupondije aina ya Scania lenye namba za usajili T798AKV mali ya Lupondije Express Kutoka Mwanza kuja Iringa kupinduka eneo la Mteremko wa Ipogolo mjini Iringa wakati basi hilo likielekea kufaulisha abiria wa Mbeya.
Alisema majeruhi 38 walifikishwa hospitali ya Iringa ambapo 11 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 27 wamelazwa wachache wakiwa mahututi.
Wema Zuberi ni mmoja kati ya majeruhi wa ajali hiyo aliyekuwa ametoka mkoani Dodoma kuelekea Mbeya aliueleza kuwa mwendo wa basi hilo toka amepanda Dodoma kuja Iringa haukuwa mkali sana kwani ulikuwa ni mwendo wa kawaida .
Japo alisema kuwa baada ya kuingia mjini Iringa katikati ya mji ndipo dereva wa basi hilo alionyesha kuendesha basi hilo kwa mwendo mkali zaidi kiasi cha baadhi ya abiria kulalamika mwendo huo na kutaka kushushwa ila dereva hakuweza kusikia zaidi ya kuwapuuza abiria hao.
“Abiria wengi walionyesha kumlalamikia dereva huyo kwanza kutokana na kuwapitiliza stendi pasipo kuwashusha na pili mwendo kasi ambao alikuwa akienda nao ili kufanikisha kutufaulisha abiria tuliokuwa tukielekea Mbeya “
Alisema kabla ya kufika eneo hilo ambalo basi lilipinduka kuna kona kali na mteremko mkali na kilichoonekana haraka haraka ni dereva kushindwa kukata kona hiyo baada ya Breki kufeli na hivyo kulazimika kuhama njia na kugonga kingo za barabara hiyo na kupinduka
RPC Kakamba aliwataja waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo kuwa ni Banenda Helen (45) raia wa Kongo, Mbuyi Leoni (52) raia wa Kongo, Jojina Nyamboko (26) mkazi wa Songea, Magambo Masunga (51) mkazi wa Mwanza, Felister Mwinuka (19) mkazi wa Njombe, Tubilisiusy Selestine (33), Said Kitonyi (17), Richard Bett (33) raia wa Kenya na Jofa Abonga
(30)mkazi wa Geita.
Wengine ni Victor Lameck (25), mkazi wa Kagera, Pius Samwel (20) mkazi wa Mara, Michael Hadu (46) mkazi wa Madaba Songea, Hassan Mfaume (20) mkazi wa Iringa, Heriet Mwitinda (29) mkazi wa Arusha, Kiliana Kalinga (22) mkazi wa Mbeya, Hima Kifyasi (32) mkazi wa Bariadi, Omary Hassan (35) mkazi wa Makambako, Zuo Pawa (30) mkazi wa Mbeya, Chacha John (26) mkazi wa Iringa.
Wengine Timoth Sichoni (24) mkazi wa Dodoma, Ishimwe Jasmin (9) rais wa Rwanda, Mkagasana Sarafina (41) rais wa Rwanda, Zaina Kisaka (26) mkazi wa Manyara, Sara Sichone (26) mkazi wa Mwanza, Ivon Magaiwa (22)mkazi wa Mafinga, Solomoni Angolisye (58) mkazi wa Dodoma, Ivan
Huwen (33) na mwingine ambaye hajajuliakana jina kutokana na kuwa na hali mbaya.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva na kuwa dereva wa basi hilo alikimbia mara baada ya ajali kutokea na kupitia mwajiri wake wanaendelea kumtafuta dereva huyo ili kuja kujibu tuhuma zinazomkabili
Akizungumza katika eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela alisema kuwa zoezi la kuendelea kutafuta miili iliyobanwa na basi hilo imekuwa ngumu kutokana na kukosekana kwa gari la kuinua basi
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kuanzia sasa dawa ya madereva hao ni kuwashughulikia kwa uzembe wanaofanya kwani kama Rai imekwisha tolewa mara nyingilakini bado ajali zinaendelea kutokea

0 comments:
Post a Comment