Freeman
Mbowe, mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) amesema kuwa, umoja huo kamwe hautaomba Umeya wa Jiji
la Dar es Salaam bali watadai.
Amesema,
Jeshi la Polisi linafanya hujuma kwa kuzuia mikutano pamoja na kukamata
wabunge pia madiwani wa Ukawa na kwamba, hiyo ni mikakati ya kukisaidia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda uchaguzi wa umeya Dar es Salaam.
Mbowe
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema-Taifa amesema umoja huo haupo
tayari kushiriki uchaguzi wa Meya kwa kushtukiza akidai kuwepo kwa
mkakati huo.
Amesema hayo jana
Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao
Makuu ya chama hicho na kwamba, mara zote wamekuwa wakitaarifiwa kwa
kushitukiza ili wasipate muda wa kujiandaa.
“Sasa tumechoka kuwabembeleza, mara zote huwa tunafanya kwa kuheshimu maamuzi yao hata kama wanavunja katiba,” alisema Mbowe na kuongeza;
“Jana ( juzi)
wabunge na madiwani wetu walienda kwa Mkurugenzi wa Jiji kwa lengo la
kutaka kujua tarehe ya uchaguzi, lakini hatukupata, kwa kuwa tumeshaomba
hawataki sasa tutakachoamua tusilaumiane. Tumechoka kudai haki kwa
kubembeleza na sasa hatutaomba tena.”
“Tunakosa
imani na viongozi wa kiserikali na Jeshi la Polisi kwa ujumla juu ya
utendaji wake na kutokana na yanayoendelea yakiwemo ya viongozi wetu wa
chama kukamatwa tunapata wasiwasi inawezekana polisi ni vibaraka wa
(CCM),”amesema Mbowe.
Akieleza baadhi ya maazimio ya Kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichokaliwa tarehe 1 Machi mwaka huu alisema,
kilitafakari utendaji wa Rais John Magufuli na kubaini kuwa, serikali
yake inavunja misingi ya utawala bora ikiwemo na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) kushindwa kusimamia majukumu yake.
Alisema
chama kinaandaa mkutano mkubwa utakaofanyikia Mwanza ambao
utashirikisha viongozi wa nchi nzima pamoja na wabunge kwaajili ya
kujadili hali ya chama na jinsi ya kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2020.Mkutano unatarajiwa kuanza tarehe 13 Machi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment