Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kukamilisha
upelelezi haraka ili kesi inayowakabili wabunge watatu wanaotokana na
Ukawa na madiwani wao ianze kusikilizwa.
Washtakiwa hao ni pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mwita Waitara (Ukonga) na Saed Kubenea (Ubungo).
Madiwani
wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni Ephrein Kinyafu (Kimara), Manase
Njema (Kimanga, Tabata) na kada wa chama hicho, Rafii Juma.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Thomas Simba alitoa kauli hiyo jana baada ya Wakili wa
Serikali, Mbunito Aloyce kudai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa kwa
kuwa upelelezi wake haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe nyingine.
Wakili
Peter Kibatala anayewatetea washtakiwa hao, aliuomba upande wa mashtaka
kuanza kuisikiliza kesi hiyo kwa sababu washtakiwa walikamatwa haraka
haraka na usikilizaji wake uwe vivyo hivyo.
Washtakiwa
hao wanaodaiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Theresa Mmbando katika vurugu zilizotokea Februari 27,2016 Ukumbi wa
Karimjee kwenye Uchaguzi wa meya na naibu meya wa jiji la Dar es Salaam,
wanatetewa na Mawakili Peter Kibatala na John Malya. Kesi hiyo
imeahirishwa hadi Aprili 18.
0 comments:
Post a Comment