Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Eda Sanga akifungua mkutano huo wa siku moja jinsi ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga akifungua mkutano huo kwa kusoma hotuba fupi ya namna ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi.
Washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi (Hayupo pichani)
Washiriki wakiendelea na mkutano huo muda huu.
Mkutano ukiendelea
Mratibu wa kituo cha usuluhishi na upatanishi wa dawati la jinsia (CRC), Bi.Gladness Munuo akieleza jambo katika mkutano huo
Baadhi wanahabari washiriki katika mkutano huo
Mratibu wa kituo cha usuluhishi na upatanishi wa dawati la jinsia (CRC), Bi.Gladness Munuo akieleza jambo katika mkutano huo
Baadhi ya washiriki kutoka katika maeneo ya jamii wakiwa katika mkutano huo
Mratibu wa kituo cha usuluhishi na upatanishi wa dawati la jinsia (CRC), Bi.Gladness Munuo akieleza jambo katika mkutano huo.
Mada ya utangulizi
Washiriki hao katika mkutano huo
Ofisa wa TAMWA katika dawati la Jamii na Jinsia, Bi. Marcela Lungu akitoa mada namna ya madawati ya kijinsia na namna ya kumpokea mteja na namna ya kulitatua.
Baadhi ya wakuu wa madawati ya jinsia pamoja na viongozi wa TAMWA
Mkurugenzi wa TAMWA akisalimiana na wadau washiriki wa mkutano huo ambao ni wawakilishi wa wananchi
Picha ya pamoja washiriki wa mkutano wa siku moja wa namna ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
Chama
cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) leo Machi 22.2016, wanaendesha
mafunzo ya siku moja jinsi ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa
kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi mkutano
uliofunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga ambaye
ameitaka jamii kuchukua hatua ikiwemo kuachana na unywaji wa pombe
kupita kiasi kwani ni hatari kwa jamii.
Katika
mkutano huo, ambao umefadhiliwa na IOGT-NTO-Movement pamoja na
wanahabari, unawashirikisha wadau mbalimbali kutoka maeneo ya mradi
unaoendeshwa na TAMWA ikiwemo maeneo ya Kata ya Makumbusho, Saranga na
Wazo wa kupinga ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji pombe
kupita kiasi kwa wanawake na watoto.
Katia
mkutano huo TAMWA pamoja na wadau wengine wameweza kuwashirikisha wadau
wa madawati ya kijinsia, Viongozi wa dini katika jamii pamoja na
viongozi wa Serikali ya mitaa na Kata pamoja na wanahabari kutoka vyombo
mbalimbali vya Habari.
Aidha,
mambo mbalimbali yamejadiliwa katika mkutano ambapo imeelezwa kuwa
katika Kata ya Saranga na maeneo ya Mbezi matatizo makubwa
yanayoripotiwa ni pamoja na masuala ya ubakaji wa watoto na vitendo vya
kulawitiwa ambapo asilimia kubwa vimehusishwa na pombe.
0 comments:
Post a Comment