(Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog)
Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wanaosomea masomo ya Sayansi na udaktari ambao wanapambana na magonjwa ya Kisukari. Dk. Kigwangalla aliwapongeza wanafunzi hao kwa juhudi zao hizo ambapo amewahakikishia juu ya Serikali kuwa na mipango endelevu ikiwemo kuwaendeleza zaidi kwa kushirikiana na wadau na wafadhiri mbalimbali.
Dk. Kigwangalla akiagana na viongozi mara baada ya kumaliza kwa ufunguzi wa kongamano hilo linaloendelea leo na kufikia tamati hiyo kesho Machi 16.2016.
Serikali
imewapongeza wadau kwa kutoa huduma za chanjo ya ugonjwa wa Kisukari
ikiwemo kusaidia vijana wadogo wanaosomea masomo mbalimbali ya kisayansi
hapa nchini.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la tatu la ugonjwa wa Kisukari
kwa nchi za Afrika Mashariki,Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya na
Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi
Kigwangalla, amebainisha kuwa Serikali kupitia wizara hiyo ina mpango
kabambe wa kuhakikisha inapambana na tatizo la ugonjwa wa Kisukari hapa
nchini ambapo pia amewataka wadau wasichoke kushirikiana katika
mapambano hayo.
Aidha,
amewapongeza vijana walio katika vyuo vikuu hapa nchini licha ya kupata
tiba ya ugonjwa wa Kisukari, lakini kwa hali yao hiyo bado wana moyo wa
kusoma kuhakikisha wanafika mbali hivyo Serikali inajisikia faraja na
kuwataka wadau kuwa na moyo huo huo wa kusaidiana na Serikali.
Kwa
upande wao baadhi ya washiriki wakiwemo vijana wanafunzi na wengine
wakiwemo waliotoa igizo namna ya ugonjwa Kisukari jamii unavyouweka
kando, wameeleza kuwa kitendo cha dozi ya Kisukari kuuzwa kinawapa shida
watu wengi kwani wapo wanaopoteza maisha kwa kukosa pesa za kutumikia
dozi hiyo.
Hata
hivyo, walimuomba Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kuhakikisha Serikali
wanaliangalia hilo ili dozi ya Kisukari yaani Insulini, ipatikane bure
kwa watumiaji wake.
Kongamano
hilo lililozinduliwa jana Machi 14.2016, ni la siku tatu na
linatarajiwa kufikia tamati, kesho Machi 16.2016. Ambapo linajumlisha
wataalaam wa utafiti wanasayansi katika ugonjwa wa Kisukari ( pre
– congress training – applied research in diebetes) na kuandaliwa na
asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study group.
Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.
Awali
akiongea na waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo Doctor
Kaushik Ramalya, amesema wageni mbalimbali wapo katika majadiliano na
uchunguzi huo wa Kisayansi, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa
namana ya kutua matatizo yatokanayo na ugonjwa huo.
UTAFITI:
Aidha utafiti uliotolewa hivi karibuni umeonyesha kuwa katika kila
sekunde sita mtu mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa kisukari ( vifo zaidi
ya milioni 5.0 hutokea duniani). Mmoja katika watu wazima 11 ana ugonjwa wa kisukari ( watu milioni 415 duniani kote wanaishi na Kisukari).
Moja
katika vizazi saba, huadhirika na ugonjwa wa kisukari katika kipindi
cha ujauzito na kujifungua.Robo tatu (75%) ya watu wenye ugonjwa wa
kisukari wanaishi katika nchi chini na kipato cha kati.
Zaidi
ya watu wazima wengi wanakufa kutokana na ugonjwa wa kisukari kuliko
kutokana na VVU / UKIMWI, kifua kikuu na hata malaria.wastani wa milioni
14.2 watu wazima wenye umri kati ya 20-79 wana ugonjwa wa kisukari
katika Kanda ya Afrika.
Afrika
inaongoza kwa wagonjwa wa kisukari ambao haujatambuliwa, kutokana na
kutocheki afya zao; zaidi ya 66.7 % ya watu wenye ugonjwa wa kisukari
hawajui kuwa wana ugonjwa wa kisukari.
Mtu
ana kisukari aina ya 2 (Type 2 Diabetes) anaweza kuishi kwa miaka
kadhaa bila kuonyesha dalili yoyote, madhara yanayoweza kujitokeza ni
pamoja na ugonjwa wa figo , moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa
jicho na kusababisha upofu na matatizo ya mguu na kusababisha ulema.
Mataifa
ya Afrika kwa idadi kubwa ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja
na Afrika Kusini (2.3 milioni ), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (1.8
milioni ) , Nigeria ( milioni 1.6 ) na Ethiopia (1.3 milioni).
0 comments:
Post a Comment