Jeshi
la polisi mkoani Arusha jana lilifanikiwa kumnusuru meneja wa kiwanda
cha kutengeneza bidha za plastiki cha Best Pack kilichopo jijini
Arusha,Vijay Kumar raia wa India baada ya kunusurika kupigwa na baadhi
ya wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Katika
tukio hilo meneja huyo alifanikiwa kujifungia katika mojawapo ya ofisi
kabla ya kuokolewa na polisi ambao walimfikisha katika kituo kikuu cha
polisi cha kati na kumhifadhi kabla ya kumwachia kwa sababu za kiusalama
Tukio
hilo lilitokea jana katika ofisi za kiwanda hicho zilizopo eneo la Kwa
Idd nje kidogo ya jiji la Arusha ambapo wafanyakazi wa kiwanda hicho
waligoma kufanya kazi wakipinga kitendo cha kampuni hiyo kutoa tangazo
la kusitisha mikataba yao ya ajira kinyume na sheria.
Mbali
na madai hayo baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho walilalamikia
hatua ya kutoplipwa mishahara yao ya mwezi Machi pamoja na mafao
mbalimbali kama malipo ya muda wa saa za ziada pamoja na kiiunua
mgongo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho walidai
kwamba uongozi wa kiwanda hicho juzi ulibandika tangazo la kusitisha
mikataba yao ya ajira katika lango kuu la kuingia kiwandani hapo kinyume
na sheria jambo lililowastua.
Catherine
Samwel na Babaa Kibori ambao ni watumishi wa kiwanda hicho walisema kwa
nyakati tofauti kwamba mnamo machi 17 mwaka huu walifanya kikao na
uongozi kujadili malipo yao mbalimbali baada ya uongozi wa kiwanda hicho
kutaka kukifunga lakini kikao hicho hakikumaliza kwa suluhu.
Walisema
kwamba juzi majira ya asubuhi wakati wanaingia kazini walikuta tangazo
likiwataarifu kwamba mikataba yao ya ajira imesitishwa bila taratibu na
kanuni jambo lililowapelekea kuvamia ofisi ya meneja huyo wakitaka
majibu ya uhakika.
Hatahivyo,wakati
wakivamia ofisi ya meneja huyo alijitahidi kukwepa na kisha kujifungia
katika mojawapo ya ofisi kiwandani hapo ambapo baada ya muda polisi
walifika na kumchomoa kabla ya kumfikisha mbele ya mikono ya jeshi hilo
kwa sababu za kiusalama.
Akihojiwa
na mtanda huu meneja huyo alisema kwamba uongozi wa kiwanda chao tayari
umeshaandaa taratibu za malipo ya mishahara na mafao mbalimbali kwa
watumisho hao na watakwenda kuwalipa watumishi hao wiki hii.
Meneja
huyo alifafanua kwamba wameamua kusitisha mikataba ya ajira kwa
watumishi hao kutokana na kampuni hiyo kutozalisha kwa faida lakini
watazingatia taratibu zote za kusitisha mikataba hiyo.
0 comments:
Post a Comment