Wananchi
wa Zanzibar leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya
kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika October 25,2025 kutokana na kasoro
zilizojitokeza.
Katika baadhi ya vituo wananchi wamejitokeza na zoezi linaendelea vizuri huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa.
Katika kituo cha shule ya sekondari Muembeladu ambayo ina vituo sita,vituo vitano vinawatu 350 na kituo kimoja kina watu 91. Akizungumza na wanahabari, msimamizi wa kituo hicho amesema zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri katika jimbo la Jangombe .
Kwa
upande wa kituo cha skuli ya Muembeshauri nako hali ni shwari na zoezi
linaendelea vizuri ambapo katika skul hiyo vituo 11 vinatumika watu
kupiga kura.
Katika Jimbo la kikwajuni, zoezi linaendelea vizuri huku mwitikio wa watu ukiwa ni mkubwa.
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wamesema zoezi hilo limekua
rahisi na la amani tofauti na taarifa zilivyokua zinasambazwa.
Mkazi
wa Muembeshauri aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu Salum Haji ametoa
wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwani zoezi la kupiga kura
linaendelea kwa amani na utulivu.
“Ndugu zangu tusikubali kugombanishwa na watu ambao hawaitakii mema Zanzibar tusimame pamoja katika kutetea nchi yetu” amesema Haji
Wakati zoezi hilo linaendelea maduka mengi yamefunguliwa na wafanyabiashara wanaendelea na kazi kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment