Askari polisi na wasamaria wema wakisaidia kutoa maiti kutoka katika basi la Lupondije Express namba T 798 AKV kutoka Mwanza - Iringa baada ya kupinduka eneo la Mteremko wa Ipogolo mjini Iringa.
Gari la kikosi cha Zimamoto na uokoaji likiwa eneo la tukio kusaidia kuokoa maisha ya majeruhi
Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela kushoto akiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bw Peter Kakamba wakisaidia kuokoa majeruhi na kutoa maiti
WATU zaidi ya wane wakufa
papo hapo na wengine
zaidi ya 20 kujeruhiwa
vibaya baada ya
basi lenye namba za usajili T 798 AKV mali ya Lupondije Express Kutoka Mwanza kuja
Iringa kupinduka eneo la
Mteremko wa Ipogolo mjini Iringa wakati basi hilo likielekea
kufaulisha abiria wa
Mbeya.
Imeelezwa kuwa
baadhi ya abiria waliokufa
katika ajali hiyo na
majeruhi ni wale ambao
walitakiwa kushuka stendi kuu ya
mabasi ya mabasi yaendaye
mikoani mjini Iringa ila dereva
wa basi aligoma kuwashusha stendi na
kupitiliza nao kwenda Ipogolo kufaulisha abiria wa Mbeya
kwanza ndipo arudi kuwashusha
stendi.
Ajali hiyo imetokea
majira ya saa 2 usiku baada
ya basi
hilo kufeli breki katika
mteremko huo huo mkali kabla
ya kupinduka .
Wema Zuberi ni
mmoja kati ya majeruhi wa
ajali hiyo aliyekuwa ametoka mkoani Dodoma
kuelekea Mbeya aliueleza mtandao huu wa
matukiodaima Blog kuwa mwendo
wa basi hilo toka
amepanda Dodoma kuja Iringa haukuwa
mkali sana ulikuwa ni
mwendo wa kawaida .
Japo alisema kuwa
baada ya kuingia mjini Iringa
katikati ya mji ndipo dereva
wa basi hilo alionyesha kuendesha basi hilo kwa mwendo mkali zaidi
kiasi cha baadhi ya
abiria kulalamika mwendo huo
na kutaka kushushwa ila dereva hakuweza
kusikia zaidi ya kuwapuuza abiria
hao.
“Abiria wengi walionyesha
kumlalamikia dereva huyo kwanza
kutokana na kuwapitiliza stendi pasipo
kuwashusha na pili mwendo kasi
ambao alikuwa akienda nao
ili kufanikisha kutufaulisha abiria tuliokuwa
tukielekea Mbeya “
Alisema kabla ya
kufika eneo hilo ambalo
basi lilipinduka kuna kona kali
na mteremko mkali na kilichoonekana haraka haraka ni
dereva kushindwa kukata kona
hiyo baada ya Breki kufeli na
hivyo kulazimika kuhama
njia na kugonga kingo za barabara
hiyo na kupinduka .
Mkuu wa wilaya ya
Iringa Bw Richard Kasesela akizungumza na mwandishi
wa habari hizi eneo la
tukio alisema kuwa zoezi la kuendelea
kutafuta miili iliyobanwa na basi hilo imekuwa
ngumu kutokana na kukosekana kwa gari la kuinua basi hilo na
tayari amemwagiza meneja
wa Tanesco kuleta gari hilo na
iwapo dereva hayupo
basi kuamka na kuendesha
mwenyewe .
Hata hivyo alisema
kuwa kuanzia sasa dawa
ya madereva hao
ni kuwashughulikia kwani kama Rai
imekwisha tolewa mara
nyingi na bado ajali
zinaendelea kutokea.
Kamanda wa polisi
wa mkoa wa Iringa Bw
Peter Kakamba ambae pia
alikuwepo eneo la tukio kusaidia kuokoa majeruhi na kutoa maiti
katika basi
hilo pamoja na mkuu huyo
wa wilaya wananchi mbali mbali walioongozwa na askari polisi
,alisema kuwa hadi majira ya saa 5 usiku wakati tunakwenda mitamboni
bado ilikuwa ni mapema kuweza kujua
ni watu wangapi
wamepoteza maisha kwani zoezi
lilikuwa bado linaendelea.
Kamanda huyo aliahidi
kutoa taarifa mara tu zoezi hilo
litakapokamilika kwa kuinua basi
hilo na kutazama kwa kina kama kuna miili ambayo
imefunikwa chini ama lah.
Mwandishi wa
habari hizi alishuhudia
miili minne ikiwa tayari imetolewa katika basi hilo huku majeruhi wengi
wakiwa wamepata majeraha makubwa
mikononi ,miguuni na kichwani,Majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
0 comments:
Post a Comment