NA RAYMOND MINJA IRINGA
Idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa wa
kipindupindu katika tarafa ya Pawaga, wilaya ya Iringa mkoani Iringa imeongezeka na kufikia watano
baada ya mgonjwa wengine kufariki na kuzikwa jana kijiji cha Luganga.
Akizungumza na Mtanzania kwa njia ya simu
Mganga mkuu wa mkoa wa Iringa Robert Salim alisema wagonjwa watatu wamefia
kwenye vituo vya afya na wawili walifia majumbani na kufanya idadi kufikia
watano.
Awali akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema usiku wa kuamkia jana mgojwa mmoja alifikishwa
zahanati ya kijiji cha Luganga lakini baada ya muda mfupi alifariki dunia .
Kutokana na kifo hicho idadi imeongezeka na kufikia watano ambapo
awali mgonjwa wa kwanza alifariki kutoka kijiji cha Mboliboli na wa pili
alikufa wakati akiwa njiani kuelekea Ruvuma na wa tatu amefia zahanati ya
kijiji cha Luganga.
Masenza alisema mgonjwa huyo alifikishwa kwenye zahanati
hiyo kwa kuchelewa sana akiwa na hali mbaya ambapo waganga walijitahidi
kumsaidia lakini ilishindikana na hatimaye kupoteza maisha .
Alisema kuendelea kuenea kwa ugonjwa huo kunasababishwea na watu wanaokunywa pombe mafichoni na wengine
wanagoma kunywa maji yenye dawa ya water guard wakilalamika kuwa yanatoa
harufu kali
.
.
Afisa Afya wa wilaya ya Iringa Sospeter Tiara akizungumza
kwenye shughuli ya mazishi ya Mario Chaula (55) alisema ni vema wakazi wote wa
tarafa hiyo kutumia dawa ya kutibu maji ya water guard ambayo wamegawiwa au
kuchemsha maji.
Alisema pia wajitokeze haraka kwenye vituo vya afya pale
wanapoona kuna mgonjwa wanayehisi kuwa ana kipindupindu badala ya kukaa naye
nyumbani na akizidiwa ndio hukimbilia hospitali.
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Iringa Pudensiana Kisaka alisema waliougua ugonjwa wa
kipindupindu tangu kulipuka kwa ugonjwa huo ni 527.
Kisaka alisema wanatumia viongozi wa vijiji kwa ajili ya
kuhakikisha elimu ya jinsi ya kujikinga na kipindupindu inamfikia kila mwananch mmoja mmoja.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment