Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akizindua rasmi ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya Kinondoni
Baadhi ya washiriki wakiifuatilia uzinduzi huo wa ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya Kinondoni mapema leo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo zilizozinduliwa rasmi wa ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya Kinondoni mapema leo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob leo amezindua rasmi
ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6,
kati ya Kata 34 zinazotarajia kupata Tsh 200,000,000/= kila Kata
ifikapo julai, 2016.
Hadi
sasa Manispaa ya Kinondoni imepeleka katika Benki ya wananchi ya Dar es
Salaam, (DCB) Jumla ya Tsh 855,003,614017 kwa ajili ya mikopo ya
wanawake na vijana ambapo ifikapo julai 2016 ambao ni mwisho wa Mwaka
wa fedha 2015/2016 zitafikia zaidi ya Tsh 4.5 billion ambayo ni sawa na
asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa mujibu ya
magizo ya Bunge.
Benki
ya wananchi wa Dar es salaam,Tawi la Magomeni imefungua vituo 36, vya
kuratibu shughulii za Mikopo ya vikundi vya wanawake na vijana katika
maeneo mablimbali ya Kata za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ili
kuwarahisishia wananchi kupata huduma za mikopo hiyo kwa karibu.
Vikundi vilivyonufaika katika uzinduzi wa leo na kiasi cha fedha kilichotolewa:-
Stopover tsh 8,750,000/= kwa ajili ya biashara ya sabuni za Maji na Miche
Makabe tsh 5,250,000/= kwa ajili ya biashara ya utengenezaji wa sabuni na uuzaji wa Mkaa.
Mbezi luis, Tsh 7,000,000/= kwa ajili ya Nursery School, Tigo pesa, Mpesa.
Kilungule tsh 2,000,000/= kwa ajili ya Biashara ya Mitumba, genge na Saloon.
Kigogo tsh 10,000,000/=kwa ajili ya biashara ya Mama lishe, Saloon ya Kike na Kiume.
Aidha
Mstahiki Meya amewataka wanawake na Vijana kujitokeza kwa wingi ili
wapatiwe mafunzo na kupewa Mikopo kwa fedha zilizopo Benki na zile
zinazoendelea kupelekwa kwa lengo la kuwawezesha wanawake na vijana
kupata mikopo kwa utaratibu wa kuwashirikisha viongozi na watendaji
ngazi ya Mitaa na Kata.
Imetolewa na:-
MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA KINONDONI
0 comments:
Post a Comment