Mwenyekiti Bavicha Patrobas Katambi akimkabidhi moja ya vitu walivyotoa msaada akiwa sambamba na makamu mwenyekiti wa bavicha patrick ole sosopi kwa wahanga.
mwenyekiti bavicha Patrobas Kitambi akizungumza na waathirika wa mafuriko walioko kambi ya Kasanga tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa mkoani Iriringa.
Waathirika
wa mafuliko yaliyotokea katika tarafa ya pawaga mkoani iringa wamepewa msaada uliogharimu
shilingi milioni moja na laki mbili na baraza la vijana la chama cha demokrasia
na maendeleo taifa (BAVICHA).
Akizungumza
wakati wa utaoaji wa zawadi hizo makamu mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA OLE SOSOPI
amesema kuwa wataendeleo kuwasaidia kila mara wanapopata kutokana na waathirika
kupoteza makazi na chakula na kuwaomba wapokee msaada walionao.
“Nilikuwa
safarini lakini nilipata taarifa ya majanga yenu kupitia vyombo vya habari
pamoja na mitandao ya kijamii niliumia sana na ndio maana niliamua kufunga
safari kuja hapa kuwajua hali na kutoa chochote nilichonacho”.alisema
Aidha
sosopi alipa pole kwa waathirika wa mafuko na wale waliopata kipindupindu na
wale waliopoteza katika kipindi hicho kigumu na kuwaomba wananchi na viongozi
mbalimbali kuendlea kuwaombea waliopoteza maisha na waliothirika.
“Jamani
tuondoe itikadi zetu za vyama,dini na kabili katika kipindi hiki kigumu ina
paswa kuishi kwa upendo na umoja ili kutumia imani na amani tuliyonayo na
kuacha kuwatenga walioathirika”.alisema sosopi
Lakini
sosopi aliongoze kwa kusema kuwa nitaendelea kushirikiana na nyie kwa njia moja
au nyingine ili mradi mrudi katika maisha yenu ya kawaida na kusahau kama
ulimkumbwa na majanga.
Sosopi
amewashukuru wananchi waliokuwa wamejitokeza kuwa kuwa watulivu katika kipindi
hiki kigumu na kuwaambia kuwa yeye ni mbunge wa wananchi kwa kuwa walimpigia
kura nyingi sana na kumfanya kuwa mshindi wa pili nyuma ya mbunge wa sasa
wiliamu lukuvu
“Tupo
hapa kujumuika na wasamaria wema wengine katika kuwapa pole walioathirika na
maafa hayo, na tunawaombea kila la kheri waweze kurudi katika hali tulivu baada
ya kupoteza wapenzi wao na mali zao,” Alisema sosopi
Naye
mwenyekiti wa waarithirika wa mafuriko hayo ABDULI NGILI amewashukuru viongozi
wa BAVICHA na serikali kwa misaada wanayoipata na kuwaomba kuendelea kuwasaidia
kwenye maeneo magumu yaliyoharibiwa wakati wa mafuriko.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya RICHARD KASESELA amesema kuwa serikali
haijawatelekeza waathirika wa mafuriko hayo,serikali itaendelea kuwasaidia
waathirika kwa kadri inavyowezakana.
Patrobas
Kitambi ni mwenyekiti bavicha taifa ameitaka serikali kutoa misaada kwa
kufikili sio kwa kukurupuka kwa kutoa misaada ya aina moja tu wanapaswa kufanya
uatafiti wa nini wananchi wanahitaji na sio kupeleka misaada tu.
0 comments:
Post a Comment