Tuesday, March 29, 2016

COSATO CHUMI APONGEZWA NA WANANCHI WA JIMBO LA MAFINGA MJINI


mbunge wa jimbo la Mafinga mjini mkoani Iringa  Cosato Chumi akiwa na balozi wa korea  mh Geum-young song wakipata picha ya pamoja baada ya maongezi ya muda mrefu.


 na fredy mgunda,iringa

Wananachi wa maeneo mbalimbali ya jimbo la mafinga mjini wamesema utaratibu wa mbunge wao Cosato Chumi kwa kwenda kutembelea maeneo yenye kero ni dalili njema zinazoonyesha kuwa hawakufanya makosa kumchagua kuwa mbunge wao na kuongeza hatadanganywa na watendaji walioko chini yake tatizo linalosababisha viongozi wengi kutoa maamuzi yasiyo sahihi na yanayoendelea kuiathiri jamii.

Aidha wananchi hao wamempongeza mbunge wao kwa juhudi anazo zifanya za kukutana na watadau mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo lake.

“Tumeona mbunge wetu akikutana na mabalozi wa nchi tofauti tofauti na wanazungumzia maendeleo ya jimbo la mafinga mjini mfano hivi karibuni mbunge wetu alikuwa na balozi wa korea  mh Geum-young song tunajua kunakitu tutapata kutoka kwa balozi huyo”. Walisema wananchi

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mafinga mjini mkoani Iringa  Cosato Chumi  ameanza  kutimiza ahadi  zake kwa  wananchi  wa  jimbo la Mafinga mjini  kwa kufanya ziara ya kutambua matatizo ya wananchi wake na kutambua nini vipaumbele vyao.

Chumi alisema kuwa lengo la kutimiza ahadi  yake  hiyo ni kama njia ya  kuwashukuru  wana Mafinga mjini kwa kumchagua katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni pia kutimiza ahadi mbali mbali binafsi ambazo alizitoa wakati akiomba kura kwa wananchi.


Alisema ataendelea  kutimiza ahadi  binafsi zilizotolewa wakati kampeni kulingana na uwezo  wake  na zile  za  kitaifa ambazo zipo katika Ilani ya CCM atahakikisha anaikumbusha  serikali  ya CCM ili  kutimiza ahadi hizo kwa  wakati.

“Ndugu  zangu wananchi  mbali  ya  kuwa  ubunge  wangu ni  wa  mwaka mmoja  ila  tayari  mimeanza  kutimiza ahadi  bila  ya kuchelewa  na  ninawahakikishieni  sita  waangusha  nitaendelea  kufanya  hivyo  zaidi  mniombee  uzima”.alisema Chumi

Mbunge huyo ameongeza kuwa hivi karibuni anatarajia kupokea msaada wa kuchimbiwa visima vitano kwenye shule za sekondari na msingi za jimbo hilo ambapo visima viwili kwa sekondari na vitatu vya shule ya msingi,msaada huo umetoka kwa ubalozi wa korea mh:Geum-young song.

“Leo nilialikwa lunch na balozi wa korea mh:Geum-young song na tumeongea mambo mengi lakini kubwa nimeahidiwa kuchimbiwa visima vitano kwenye shule za msingi na sekondari zilizopo kwenye jimbo la mafinga mjini mungu ni mwema jambo hili likifanikiwa litatusaidia kuwapunguzia adha wanafunzi wetu”.alisema Chumi

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More