Thursday, April 6, 2017

WALEMVAU KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA KUPATIWA HUDUMA BURE PAMOJA NA MISAADA MBALI MBALI

Halmashauri ya jiji la Arusha imeahidi kutoa shilingi laki saba na ishiri  kupitia mfuko wa afya ya jamii (TIKA) kwa watu wenye ulemavu kwaajili ya kuwalipia  huduma za afya bure ndani ya mwaka mmoja kwa vituo vyote vilivyopo ndani ya jiji la hilo
 
Akizungumza katika mkutano ulIowakutanisha watu wenye ulemavu na uongozi wa halmashauri ya jiji la arusha mkurugenzi mtendaji   wa jiji la Arusha Ndg Athumani Juma Kihamia amesema kuwa lengo la kuwapatia fedha hizo kutokana na walemavu wengi ambao wamekuwa wakiosamitaji ya kufanyia kazi hali inayopelekea kundi hilo kuwa masikini.

Kwa upande wake mratibu wa mfuko wa afya ya jamii TIKA Bi Rossemary Tigando ameelezea mipango yao ambayo ni pamoja na kuhakikisha watu wote wenye ulemavu kupata huduma ya afya ndani ya mwaka mmoja  bila usumbufu wowote katika hospitali zote za halmashauri  jiji la arusha.

Aidha watu wenye ulemavu wamepongeza hatua hiyo iliyochukuliwa na uongozi wa halmashauri na kutoa wito kwa wenzao kufuata taratibu zilizotolewa za usajili wa kadi ya bima ili isilete adha kwa watoa huduma

Pamoja na kuisifia hatua hiyo kutoka kwa halmashauri watu wenye ulemavu bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na,mitaji,vifaa vya kujimudu kama miguu mikono bandia,mikopo yenye riba nafuu,kutokuwa na miundombinu rafiki na mengine mengi waliorodhesha kwenye risala yao kwa mgeni rasmi.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More