Monday, April 17, 2017

MBUNGE KABATI UKWATA LAZIMA MNUNUE BASI KWA AJILI YA MAENDELEO YETU

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati aliongea neono wakati wa harambee ya kuchangia fedha za kununulia gari kwa ajili ya maendeleo ya UKWATA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali waliokuwepo wakati wa harambee ya utafutaji wa kupata Pesa za kununulia gawa ajili ya UKWATA Mkoa wa Iringa.
Baadhi ya wanaukwata waliokuwepo siku ya harambee kutoka maeneo mbalimbali Mkoani iringa

Na Fredy Mgunda, Iringa

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati amechangia ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) iliyo chini ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) inayolenga kuwasaidia Wanafunzi wa Madhehebu ya CCT kiroho na kimaadili katika shule za Sekondari, Vyuo vya Ufundi ,Vyuo vya Elimu na Vyuo vingine vya Kanisa na vya Serikali kwa ajili wa kununua basi ambalo liatakuwa linagharimu Zaidi ya million sitini.

Akizungumza wakati wa harambee ya kutafuta Pesa za kununulia gari Mbunge Kabati alisema kuwa jamii ya kikristo inapaswa kuendelea kuwa wamoja ili kuendelea kudumisha umoja wa watanzania kwa kuwa UKWATA ni sehemu ambayo inawafundisha maadili wanafunzi ya jinsi gani ya kuishi kwa umoja na kumuabudu mungu.

"Saizi tuna vijana wengi wapo mitaani hawamjui mungu na wamekuwa wanatumia madawa ya kulevya,wengine wanatumika katika kazi za kishetani kwa kuwa wengi wao hawakupata mafunzo kutoka kanisani au msikitini hiyo viongozi na walezi wa UKWATA lazima muwekeze nguvu za kutosha ili kuikomboa jamii yetu ya kitanzania"alisema Kabati

Kabati aliwataka vijana kukua katika maadili ya kimungu kwa kuwa ndio malezi mazuri kwa mwanadamu yoyote yule hivyo tunatakiwa kuwashauri vijana wengi wanapotea kwa kuwa hao wote ni lika yenu na mnaishi na kucheza pamoja.

Suluhisho la changamoto zinazowakabili Vijana ni kama jamii na wadau mbalimbali wa Maendeleo kama serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserekali ( NGO’s), Kanisa na Vijana wenyewe wataweza kuona changamoto hizi na matokeo yake kisha kufikiri njia za kukabiliana nazo. 

Vijana wakitambuliwa, wakihamasishwa, kuwezeshwa na kupewa elimu na maadili bora katika maeneo yote na nyanja zote, tatizo litapungua kama si kwisha kabisa. Wachungaji na wote wanaopenda maendeleo ya Vijana wanao wajibu wa kuhimiza Uinjilisti kwa vijana, huduma ya ushauri na utunzaji hali kadhalika kutenga muda wa Neno na Maombi na Vijana ikiwezekana mara moja kwa mwezi itasaidia sana kupunguza tatizo.

Kwa baadhi ya walezi walikuwepo katika harambee hiyo walimpongeza na kumshukuru Mbunge Kabati kwa jitihada anazozifanya kuisadia jamii kwa kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali hapa Mkoani iringa na Tanzania kwa ujumla.

Lakini walezi hao wa UKWATA waliomuomb mbunge huyo kuwasidia kufanikisha lengo lao la kununua gari aina ya basi hata kwa kuwaombea kwa wabunge na viongozi wengine kwa kuwa uwezo huo anao.



"Leo mbunge Kabati ametuchangia shilingi million moja kwa hiyo tukienda kwa viongozi wengine najua tutapata Zaidi kwa kuwa yeye pia ni Mwenyekiti wa wabunge wote wa Mkoa wa Iringa hivyo itakuwa njia rahisi kutufanikishia adhima yetu hata hivyo tunamshukuru kwa kuwa nilikuwa ghafla sana ila amekuja na katuchangia tunamshukuru na tu naomba mungu ambariki katika kazi zake" walisema walezi wa UKWATA mkoa wa Iringa.



Nao baadhi ya viongozi wa UKWATA Mkoa wa Iringa walisema kuwa Malengo Makuu ya UKWATA ni kuwasaidia Wanafunzi wawe na msingi bora wa maisha ya kiroho kwa njia za Ibada za pamoja,Vipindi vya kujifunza Biblia, Maombi, Sala. Chini ya UKWATA, Vijana Mashuleni huimarishwa kuiga tabia ya Yesu Kristo katika kudumisha Umoja, kuhudumiana kiroho na kimwili wao kwa wao, pia kuwa na maandalio ya Kikristo na kutiwa moyo katika kulitumikia Kanisa.


Viongozi wa UKWATA walimshukuru mbunge Kabati kwa kuwa changia kiasi cha fedha ambazo zinawafanya waamini kuwa siku moja watatiza malengo yao ya kununua basi ambalo kitakuwa msaada kwao na kuondokana na kuwa omba omba.





0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More