Saturday, April 22, 2017

DC UBUNGO ASULUHISHA MGOGORO WA ARDHI GOBA

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Kisare Matiku Makori  amesuluhisha mgogoro wa ardhi  uliokuwepo kati ya wakazi wa Mtaa wa  Kulangwa na Tegeta A Kata ya Goba   kwa kuamuru kusimama kwa mpango wa upimaji wa maeneo yenye mgogoro uliokuwa unafanywa na familia ya Seif Ngane  na badala yake  kuwapatia maeneo yao wakazi waliopewa maeneo hayo na serikali ya kijiji katika mitaa ya Kulangwa na Tegeta A Kata ya Goba

Agizo hilo amelitoa leo wakati wa mkutano kati ya pande zote zilizokuwa na mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.

Mgogoro huo wa ardhi unaohusisha familia ya Seif Ngane na wananchi waliopewa maeneo na serikali ya kijiji kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa wakati huo ndugu Yusuph Makamba unahusisha umiliki wa eneo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa ekari  99

Akizungumza wakati wa mkutano huo  Mkuu wa Wilaya alisema;-

"Wote waliopewa maeneo na serikali ya kijiji na wana ushahidi wa maandishi wapeleke vielelezo vyao kwenye ofisi za Serikali ya Mtaa na Kata  ili kuhakiki vielelezo hivyo kama sehemu ya mchakato wa kupimiwa maeneo hayo na kupatiwa   Hati ya umiliki   wa eneo husika" alisema .

Aidha, Mhe. Kisare  ameagiza wale wote wanaoendelea kutumia maeneo ya ardhi ambayo Seif Ngane alishinda kesi dhidi yao Mahakamani wasitishe kuyatumia mara moja  na  wasiyaendeleze maeneo hayo" .

"Kuhusu eneo ambalo Seif Ngane  alimuuzia Ndg. Octavian William Temu,  Mhe Kisare ameelekeza pande mbili zinazohusika kukutana ofisini kwake  Alhamisi wiki ijayo kwa sababu pande zote mbili zimeshindwa kuthibitisha kwa  vielelezo kiasi cha ardhi walichouziana.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi waliokuwa na mgogoro huo Mwenyekiti wa kikundi hicho Ndg. Venance Mhingwa alimshukuru sana Mkuu wa Wilaya kwa busara aliyotumia na hatimaye kutoa maamuzi ya haki kwa pande zote zilizokuwa na mgogoro huo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More