Wednesday, April 5, 2017

VIONGOZI WATATU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUHUJUM UCHUMI

Inline image 1
NA MZIDALFA ZAI(ARUSHA)

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kwa kushirikiana na Wakili wa Serikali wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora imewapandisha kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Igunga viongozi watatu wa serikali ya Kijiji cha Isenegeja kwa tuhuma za wizi wa fedha za serikali.

Waliopandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Isenegeja,Ahmed Jambeck(50),Mjumbe wa serikali ya Kijiji cha Isenegeja,Seleli Kashindye (58) na aliyekuwa Kaimu afisa Mtendaji wa Kijiji cha Isenegeja Michael John (47) wote wakazi wa kijiji hicho.

 Awali Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)kutoka Mkoani Tabora,Edson Mapalala wakishirikiana na wakili wa serikali kutoka Mkoani Tabora,Tumaini Pius alida kuwa washitakiwa wote watatu wanashitakiwa kwa makosaa mawili likiwemo la wizi wakiwa watumishi wa serikali ya Kijiji cha Isenegeje huku shitaka la pili likiwa ni wizi.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo,Ajali Milanzi,Mwendesha Mashataka huyo alidai kwamba washitakiwa hao walitenda kosa hilo kati ya mwaka 2008 na 2015 wakati wakiwa watumishi katika Kijiji cha Isenegeja kwa pamoja waliiba shilingi 34,131,000/= mali ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo Mapalala alidai Mahakamani hapo kuwa baada ya washitakiwa hao kufanya wizi huo,walibadilisha matumizi yao binafsi ya fedha hizo bila kuwa na kibali cha kufanya hivyo.

Aidha Mwendesha Mashitaka alidai Mahakamani pia kwamba washitakiwa walitenda kosa la kwanza kinyume na kifungu 271 cha kanuni ya adhabu sura 16 mapitio ya 2002 na kosa la pili walitenda kinyume na kifungu 258, 1, 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashita hayo mawili,washitakiwa wote watatu wamekana kutenda makosa hayo na kwamba wote wapo nje kwa dhamana ya shilingi milioni 35 kila mmoja hadi Apr,19,wmwaka huu kesi hiyo itakpotajwa tena.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More