WACHIMBAJI
wadogo wa madini waliopotea kwa kufunikwa na kifusi kwenye mgodi wa
Nyangarata, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 5 mwaka wamepatikana, watano
wakiwa hai na mmoja akiwa amefariki.
Taarifa
hiyo imetolewa leo na Afisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini,
Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
wachimbaji hao ambapo amesema kuwa waliishi chini ya mgodi huo kwa muda
wa siku 41 wakila magome ya miti na maji yanoyotelemka kwa nadra.
Masoud
amesema kuwa wachimbaji walikuwa sita ambapo watano waliokolewa wakiwa
hai baada ya kusikika na wachimbaji wa mgodi wa jirani na mgodi huo
wakiomba msaada kwa ishara ya kugonga kuta za mgodi huo ndipo walipo
watambua na kuitwa msaada ambapo mmoja kati ya hao alifariki dunia na
kushindwa kutolewa katika mgodi huo.
Akitaja
majina ya wahanga hao ni Muhangwa Amosi, Joseph Bulule, Chacha Wambula,
Unjiwa Aindo, Msafiri Gerald na aliyefariki ni Mussa Supana.
Mosoud
amesema kuwa wachimbaji hao watano walionusurika kufa wamelazwa kwenye
hospitali ya wilaya ya Kahama na hali zao bado sio nzuri ambapo amesema
kuwa wizara itaendelea kutoa taarifa zaidi za wahanga hao.
Wizara
ya Nishati na Madini wamewata wachimbaji wadogo watumie mfumo na dhana
bora za uchimbaji wa madini ili kujihakikishia usalama wao.
0 comments:
Post a Comment