Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ametoa ufafanizi wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuhusu kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika Wizara,idara na Taasisi za serikali.
Katika ufafanuzi huo,Balozi Sefue amemtaka kila Mtendaji Mkuu ama Afisa Masuhuli wa serikali kujiuliza mwenyewe ni kwa kiasi gani anatekeleza kwa vitendo nia ya Rais ya kuepuka matumizi yasiyo ya lazima
"Rais
ameonesha njia, sasa kwa wakati huu ni vema kila mtendaji mkuu wa
serikali,ajiulize endapo Rais atafika katika eneo langu la kazi,ni kwa
kiasi gani atakuta nimetekeleza maagizo yake?" Amesisitiza Balozi Sefue
Kutokana
na ufafanuzi huo, Blozi Sefue pia amezungumzia uchapishaji wa kalenda
na vitabu vya kumbukumbu yani "Diaries" akisema kila mtendaji mkuu wa
Serikali ama Afisa Masuhuli apime mwenyewe kama ni lazima kutengeneza au
kuchapisha kalenda na Diary? na kama ni lazima achapishe kwa kiasi
gani?
"Ni
matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kila wizara,Idara na Taasisi za
serikali kuchapisha idadi kubwa ya kalenda na Diaries ambazo wakati
mwingine hata hazitumiki mpaka mwaka unakwisha." Ameongeza Balozi Sefue
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
0 comments:
Post a Comment