Thursday, November 26, 2015

ASKOFU MDEGELA AMESEMA KUWA CCM HAIJAWI KUSHINDA ZANZIBAR TOKA MFUMO WA VYAMA VINGI UANZE.

askofu akanisa la kilutheri mkoani iringa   Dkt. OwdenburgMdegela amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani yetu baada ya uchagumzi mkuu umalizike kwa upande wa tanzania bara..
akizungumza na watangazaji wa nuru fm katika kipindi cha sunrise power  wakati wa uchambuzi wa maswala ya kisiasa,mdegela alisema kuwa chama cha mapinduzi (ccm)hakijawahi kushinda kule zanzibara na kusema kuwa mwaka huu maarim seif shariff hamadi
“hata ukininukuu nitaendeleea kusama hivi hata kama ukiniandika kwenye magazeti,tangu vianze vyama vingi zanzibar chama cha mapinduzi (ccm) pengine hawajawawi kushinda na uchaguzi hajawahi kuwa sahihi” alisema askofu mdegela
askofu mdegela alisema kuwa ccm  mwaka huu matokeo yalikuwa wazi zaidi kuwa seif shariff hamadi alikuwa ameshinda lakini alinyang’anywa ushindi mikononi na kuzipoteza kura zake mchana kweupe
lakini ameitaka tume yauchaguzi ya zanzibari imtangaze seif kuwa ndiye mshindi wa zanzibar na chama cha mapinduzi (ccm) wanatakiwa kukubaliana na matokeo hayo na kuacha figisufigisu wanazoziendeleza huko .
aidha askofu mdegela alisema angalau tumepata rais ambaye atatusaidia kuirudisha nchi kwenye nidhamu ya kuleta maendeleo kutokana na hotuba yake na mwanzo wake .
“wananchi walikuwa wamechoka na kukata tamaa juu ya serikali yao na walikuwa tayari kuweka jiwe na kulipigia kura kuliko kumchagua kiongozi kutoka chama cha mapinduzi(ccm)” alisema askofu mdegera
nchi hii demokrasia bado haijafika pale inapotakiwa kwa kuwa watu wengi wananyanya swa pale wanapoenda tofauti na cha tawala hiyo sio demokrasia  bali hizo ni figisufigisu za kijinga.
ameongeza kuwa hamfahamu hata kidogo waziri mkuu wa sasa lakini ni mwanafunzi wa prof moja anayefundisha chuo kikuu cha iringa zamani tumaini alisema anawezaweza bado muda hebu tumuangalie utendaji wake wa kazi.
Amewapongeza wananchi  kwa kuwa watulivu kipindi cha kupokea matokeo hadi pale tulipompata rais wa jamhuri ya muungano kwa kuitunza amani.
“Hata nikiwa wapi ntaendelea kijidai kwa kuwa wananchi wa nchi yangu ni watunza amani na hata kama kunatatizo kuna njia nyingine ya kupata haki kwa kuwa kuna sheria zinazostahili kupta haki”.alisema askofu mdegela
Mdegela alimalizia kwa kusema  kuwa ccm hawataki mshilazi atawale nchi ya zanzibar  kwa kuwa mwendo unaoendelea sio wa kidemokrasia ili wananchi wa Zanzibar wanaijua siasa yao zaidi. 

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More