Aliyekuwa
mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR
-Mageuzi, David Kafulila, amewasilisha pingamizi katika Mahakama Kuu
Kanda ya Tabora, kupinga ushindi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Hasna Mwilima.
Akizungumza na mtandao huu
jana baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Kafulila alisema amefungua
kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015 ya uchaguzi, akiwalalamikia Mwilima,
msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza na
Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Alisema
kesi hiyo itasimamiwa na mawakili wawili, Tundu Lissu na Daniel
Lumengela, huku hoja ya msingi katika shauri ikiwa ni kupinga matokeo
yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi ambayo anadai si halali kwani
kutokana na fomu 382 za vituoni na kusainiwa na wasimamizi na mawakala,
alipata kura zaidi ya 34,000 dhidi ya 32,000 za mpinzani wake (Mwilima).
0 comments:
Post a Comment