JUMLA ya
kaya
201,120 ambayo
ni sawa na asilimia 89 mkoani Iringa zina vyoo na
kati ya Kaya hizo asilimia 17 tu ndiyo
zenye vyoo bora.
Kauli hiyo imetolewa jana
na katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo
ya kuhamamisisha wanahabari juu ya usafi wa mazingira.
Ayubu amesema kuwa lengo la
mafunzo hayo ni kuwa kuwajengea uwezo wanahabari kujua
mambo muhimu yanayohusiana usafi wa mazingira na matumizi ya choo ikiwa
ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira hapa nchini.
Amesema kuwa hali ya unawaji
mikono
kwa sabuni
ni sawa na asilimia tisa huku hali ya
matumizi ya choo na unawaji wa mikono kwa sabuni bado vikiwa
bado vipo chini.
Naye ofisa afya wa mkoa wa
Iringa Khadija Haroun amesema mafunzo hayo
yanaenda sambamba na wiki ya usafi wa mazingira hapa nchini.
Haroun amesema kuwa watu takriban milioni 1.8 wanakufa kila mwaka duniani
kote kutokana na magonjwa ya kuhara.
Amesema kuwa watoto chini ya miaka mitano 760,000 hufa kila mwaka kutokana na magonjwa
ya kuhara kila mwaka.
Pia amesema kuwa tanzania watu 30,000 hufa kila mwaka kutokana
na magonjwa ya kuhara.
Amesema kuwa asilimia 60 hadi 80 ya wagonjwa wote wa
nje wana magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji na mazingira machafu.
Naye
Ofisa habari wa mkoa wa Iringa Dennis Gondwe
amewataka wanahabari mkoani hapa kutoa
elimu kwa jamii kuhusu mafunzo waliyoyapata katika mafunzo hayo ambapo alisema
kwa kupitia waandishi wa habari jamii itapata elimu itakayowasaidia kuweza
kuepukana na ugonjwa wa kuhara pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.
0 comments:
Post a Comment