Ongezeko la watu wanaojihusisha na mapenze ya jinsia moja maarufu kama ushoga linazidi kwa kasi mkoani Iringa
Hayo yamesemwa na mkuu Wa mkoa Wa Iringa bi. Amina Masenza alipo kutana na viongozi Wa dini, viongozi Wa siasa na wazee Wa mkoa huo kwenye mkutano wenye lengo la kuboresha lishe bora na jinsi ya kumaliza au kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi mkoani iringa
Masenza amesema baadhi ya wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wengine ni watu wenye nyadhifa zao na wakuu Wa vitengo mbalimbali na kutumia kipato chao kuwarubuni vijana
Masenza amesema hali ya maambukizi ya ukimwi Iringa bado ni mbaya licha ya malengo yaliyowekwa na ofisi yake kuwa hadi ifikapo mwaka 2018 udhibiti Wa maambukizi yawe kwa asilimia mia moja
Baadhi ya washiriki Wa mkutano huo wamesema serikali iweke muda maalum Wa kufungua sehemu za starehe kama vile bar, vilabu vya pombe, club nk kwa sehemu hizo hufunguliwa asubuhi na mapema na kusababisha watu kunywa na kulewa asubuhi
"Mkuu Wa mkoa na mkuu Wa wilaya naombeni niwapeleke mitaa ya kitanzini au mitaa ya kihesa yaani ikifika saa mbili asubuhi wamama, wababa, vijana wapo tilalila hoi taabani, afu ndio tunasema ukimwi utaisha tunaomba mshughulikie utaratibu Wa kufungua hizi bar bila hivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu" alisema kiongozi mmoja Wa kidini aliye hudhuria mkutano huo
Richard Kasesela ni mkuu Wa wilaya ya Iringa amesema ataanza na kuzifungia sehemu zote za starehe zisizo na Kibali maalum pia kuhakikisha night club zote zifate sheria kwa kuhakikisha zinanakuwa na Kibali maalum na kuwa sound proof kudhibiti sauti kutoka nje ya club kubughdhi watu wengine
Kasesela amewaonya watu wanao warubuni mabinti wadogo kwa vijisenti na kusema wamejipanga kutumia mbinu maalum za kuwabaini watu hao
Ikumbukwe iringa ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kitaifa kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi.
0 comments:
Post a Comment