Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akitoa taarifa kwa wananchi baada ya Chadema Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema leo kimefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, ili kuiomba
Mahakama hiyo kutengua zuio la kuuaga mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa chama
hicho Mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo, lililotolewa na Jeshi la Polisi
Mkoani Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa ugonjwa wa
Kipindupindu.
Katika kesi
hiyo, Chadema inawakilishwa na Mawakili watatu ambao ni James Millya, John
Mallya pamoja na Paul Kipeja ambapo mlalamikaji ni Charles Lugiko ambae ni baba
mdogo wa Marehemu Mawazo.
Mahamaka
hiyo chini ya Jaji Lameck Mlacha, imesikiliza malalamiko ya upande wa washtaki
na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo imeamuru mlalamikiwa ambae ni Mkuu wa
Polisi Mkoa wa Mwanza pamoja na mwanasheria Mkuu wa Serikali kupelekewa nyaraka
za kesi hiyo kabla ya kusikiliza utetezi wao hapo kesho.
Mapema kabla
ya kesi hiyo kusikilizwa, wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika nje ya
viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, walilalamikia hatua ya jeshi la polisi
kuwazuia kuingia Mahakamani hapo ili kujua hatima ya kesi hiyo, ambapo wamesema
kitendo hicho kinaondoa dhana ya Rais John Pombe Magufuli, kuwa yeye ni rais wa
wananchi wote wakati wao kama Chadema wananyimwa haki zao.
Licha ya
Malalamiko hayo pamoja na ulinzi mkali wa polisi uliokuwa umetanda Mahakamani
hapo, bado wafuasi wa Chadema hawakuondoka katika viunga vya Mahakama hiyo hadi
pale Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe alipowasihi kurejea
majumbani mwao hadi kesho kesi hiyo itakaposikilizwa tena.
Ni zaidi ya
siku nane sasa tangu marehemu Alphonce Mawazo auawe kikatili Mkoani Geita na
watu wasiojulikana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni chuki za kisiasa
ambapo mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Mmoja wa Mawakili wa Chadema John Mallya akitoa taarifa kesi baada ya Chadema Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.
Kesi ilisikilizwa katika Jengo la Mahakama ya Biashara lililopo katikati ya Jiji la Mwanza. Pichani ni mawakili wa Chadema wakielekea mahakamani huku kukiwa na umati wa wafuasi wa Chadema (Ukawa) pamoja na viongozi waandamizi wa Chadema

Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo

Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo.
0 comments:
Post a Comment