POLISI
mkoani Morogoro inawashikilia watu watatu, wakazi wa Manispaa ya
Morogoro na Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kusafirisha matenga
manane ya bangi iliyohifadhiwa pamoja na ndizi.
Bangi
hiyo ilikuwa ikisafirishwa katika gari kubwa iliyokuwa ikitokea mkoani
Singida kuelekea Dar es Salaam na miongioni mwa wanaoshikiliwa ni pamoja
na dereva wa gari hilo, Venance Patrick (44), mkazi wa Kiwanja cha
Ndege, mjini hapa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema jana kuwa watuhumiwa
hao walikamatwa Novemba 21, mwaka huu saa tisa usiku katika eneo la
mizani Mikese katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Kamanda Paulo, Patric alikuwa akiendesha gari namba T 269 BJN
aina ya Volvol Semi yenye tela namba T 215 AGC. Aliwataja watuhumiwa
wengine kuwa ni Jumanne Makila (28) mkazi wa Kiwanja cha Ndege na Juma
Mbaraka (30) mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam.
Kamanda
huyo alisema, askari waliokuwa katika operesheni maalumu barabara kuu
walifanikiwa kukamata gari na watuhumiwa hao wakiwa na bangi ndani ya
gari yenye uzito wa kilo 120 ikihifadhiwa kwenye matenga manane kwa
kuchanganywa na ndizi mbichi. Alisema polisi wakikimilisha upelelezio
watawafikisha mahakamani watuhumiwa hao.
0 comments:
Post a Comment