Rais
wa Kenya, Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri
na kuwapiga chini mawaziri wote ambao wizara zao zinakumbwa na kashfa za
ufisadi.
Uamuzi
wa Rais Kenyatta umekuja siku moja baada ya kutangaza ufisadi kama
tishio la usalama wa kitaifa huku akiazimia kufanya mabadiliko makubwa
kwenye ofisi ya Rais hivi karibuni.
Katika
mabadiliko hayo, Kenyatta ameongeza pia idadi ya wizara kutoka 16 hadi
20 na kuongeza idara mpya chini ya wizara hiyo, kutoka idara 26 hadi 41
kwa kile alichoeleza kuwa ni kusaidia wizara kutekeleza majukumu yao
bora zaidi.
Baadhi
ya mawaziri walikuwa tayari wamekwisha jiondoa kwenye wizara zao kwa
tuhuma za ufisadi huku wengine wakiwa na kesi za kujibu mahakamani.
Hivi
karibuni, Waziri wa Ugatuzi, Anne Waiguru alikuwa wa mwisho kujiondoa
kwenye wizara akiwa na kashfa zilizopata umaarufu zaidi kwa kipindi cha
hivi karibuni za kununua kalamu moja kwa shilingi zaidi ya 200,000 za
Tanzania.
Hata
hivyo, Uhuru Kenyatta hakuwa na budi ya kuvunja baraza lake na kuunda
upya kwa kuwa katiba ya nchi hiyo inataka idadi ya mawaziri isiwe chini
ya 14. Baada ya Waiguru kujiuzulu nafasi ya uwaziri, baraza la mawaziri
lilibaki na mawaziri 13 pekee.
0 comments:
Post a Comment