BAADHI ya wanaume
nchini, wametajwa kuwa chanzo cha ongezeko la vifo vya wanawake, vitokanavyo na
saratani ya shingo ya kizazi, kwa madai ya kuwazuia wenza wao kwenda kupima ugonjwa
huo ambao umeonekana kupoteza uhai wa akinamama walio wengi.
Hayo
yamezungumzwa na akinamama waliohudhuria huduma ya uchunguzi wa Saratani ya
shingo ya Kizazi, mpango ulifadhiliwa na kampuni ya Green Resources –
inayojihusisha na shughuli za upandaji wa miti katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Flaviana Myovela na Mayasa Hassan ni
baadhi ya akinamama waliohudhuria huduma hiyo, wamesema mwamko duni miongoni
mwa wanawake wenzao, unatokana na baadhi ya wanaume kuwazuia wake zao kushiriki
huduma ya uchunguzi wa saratani hiyo, wakidhani mpango huo umelenga kuwafunga
vizazi wake zao.
Hongera
Kiyungu na Olester Mkweve wamesema ili
kukabiliana na fikra hizo potofu, serikali inalojukulu la kuwapatia elimu wanaume, juu ya madhara yatokanayo na
ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, ili waachane na fikra potofu ambazo
kwa namna moja au nyingine zinachangia ongezeko la vifo vya wanawake.
Hata hivyo Rose
Marick - mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Green Resource Tanzania, amesema
sababu ya kusogeza huduma hiyo ni kuwapunguzia umbali wa kuifuata huduma hiyo,
huku akitoa ushauri kwa akinababa wenye imani potofu juu ya huduma hiyo, kwa
madai kuwa kulifumbia macho tatizo hilo ni kuchangia ongezeko la vifo kwa
wanawake.
Zoezi hili la
uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wafanyakazi wa kampuni ya Green
Resources wilayani Mufindi na jamii
inayoizunguka kampuni – limewalenga kuwafanyia uchunguzi wanawake zaidi ya 2000 – ugonjwa ambao kwa
mujibu wa takwimu za madaktari – wanawake 11 Tanzania kila siku hufariki kwa
ugonjwa huo.
Mpango huo wa kusogeza zoezi la upimaji wa
Saratani ya shingo ya Kizazi kwa wanawake utawanufaisha kundi hilo la
wafanyakazi na wananchi wa eneo hilo la Twico, kwakuwa baadhi yao
hushindwa kuifuata huduma hiyo katika Hospitali ya Mafinga ambayo ipo
umbali wa km 15 kutoka katika eneo la Kiwanda.
0 comments:
Post a Comment