Monday, November 16, 2015

KAULI ZA LOWASA,MBOWE,ZITTO KABWE NA WENGINE JUU YA KIFO CHA ALPHONCE MAWAZO ZIKO HAPA NA RIPOTI NZIMA YA KIFO CHAKE

Freeman Mbowe
Mwenyekiti wetu wa Mkoa wa Geita na aliyekuwa Mgombea wetu wa Ubunge jimbo la Busanda Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo ameuwawa leo huko Katoro Busanda. Alikuwa mpiganaji jasiri na makini. Hakika tumepoteza nguzo muhimu Kanda ya Ziwa. Chama kimepokea kwa mshtuko mkubwa kifo hiki ambacho tunaamini kimepangwa. Tunavitaka vyombo vya dola vitupe taarifa kamili ya wahusika wa unyama huu. Nawapa pole Wanachadema wote, ndugu na Jamaa.

Edward Ngoyai Lowassa
Nimeshtushwa na kusikitishwa na taarifa za msiba wa kijana wetu Alphonce Mawazo, Natoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na familia yetu ya UKAWA.
Hakika tumeondokewa na mpiganaji.

Zitto Z Kabwe
Nimeshtushwa sana na mauaji wa ndg. Mawazo mwenyekiti wa CHADEMA Geita. Mauaji haya lazima yachunguzwe na hatua stahiki zichukuliwe
Muslim Hassanali
R.I.P kamanda Alphonce Mawazo. Natoa Pole kwa Ndugu,Marafiki, Wanachama wa Chadema/ UKAWA na Wananchi wa Busanda, Kwa Niaba ya Bodi Ya Wadhamini wa Chadema-Taifa, Tumepokea kwa Mshtuko mkubwa taarifa ya Kifo cha Kamanda Wetu Mwenyekiti wa Geita na ambaye pia alikuwa Mgombea Ubunge - BUSANDA. "We have Lost the Battle, Not the War" Inna Lillahi, wa inna illaihi Rajioon. (Kny ya Bodi ya Wadhamini): Muslim Hassanali- Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini Chadema-Taifa.

Julius S. Mtatiro
ALPHONCE MAWAZO????
Ndugu zangu, nimejulishwa ati Mwenyekiti wa CHADEMA wa mkoa wa Geita, kamanda Alphonce Mawazo amefariki dunia leo.
Taarifa zinaoneshwa kuwa alivamiwa jana na kukatwa mapanga vibaya akiwa kwenye harakati za uchaguzi wa udiwani huko Geita.
Mawazo, ni kweli umekwenda? Hivi hivi!!!
Mwenye taarifa kamili na rasmi na atupatie hapa.
Mungu wangu!
Mtatiro J.
STORY KWA UFUPI ILIKUWA HIVI
Afande  mkoa wa Geita kuna tukio la mauaji KTR/IR/1186/2015, lililotokea leo tarehe 14/11/2015 baada ya ALPHONCE S/O MAWAZO, miaka 39, msukuma, mkulima mkazi wa Geita na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita pia katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa mgombea ubunge jimbo la Busanda, alishambuliwa kwa silaha za jadi na watu wanaosadikiwa kuwa zaidi ya kumi kati yao mmoja ametambuliwa kwa jina moja la MABEGA, wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa CCM. 
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa CHADEMA walikuwa na mkutano wao wa ndani katika mtaa wa Ludete A kata ya Ludete katika mji mdogo wa Katoro na CCM pia walikuwa na mkutano na ndani katika ofisi ya CCM, mtaa wa Njiapanda kata ya Ludete, vyama vyote viwili vilikuwa vinaandaa na kuwaapisha mawakala wao kwa ajili ya uchaguzi wa diwani ambao utafanyika kesho tarehe 15/11/2015 katika kata ya Ludete.

Wakati mkutano wa chadema ukiendelea majira ya 12:35 hrs mwanachama mmoja wa CHADEMA alitoa taarifa kuwa nje ya ukumbi kuna watu wanaosadikiwa kuwa wanachama CCM wanarekodi mkutano wao. Baada ya taarifa hiyo wajumbe wote walitoka nje ya ukumbi wakakutana na  kundi la hilo nje ya ukumbi. Watu hao waliwashambulia kwa silaha butu 1. ELIZABERT D/O PASCHAL, miaka 43, msukuma, mkulima wa Katoro ameumia kisogoni 2. BAHATI S/O MICHAEL, miaka 38, mzinza, mkulima mkazi wa Katoro, amejeruhiwa kichwani. Wametibiwa kituo cha afya Katoro, wameruhusiwa na hali zao zinaendelea vizuri. Kutokana tukio hilo wajumbe wote wa CHADEMA walitawanyika.
Marehemu alitoweka katika eneo hilo katika mazingira ambayo hata wenzake wameshindwa kuyaelezea. Muda mfupi alionekana akipigwa katika umbali unaokadiliwa kuwa nusu kilometa kutoka ukumbi ulipokuwa unafanyika mkutano wao na watu kumi walioshuka kwenye gari aina ya Land  Cruiser ambayo namba zake bado hazijafahamika. Baada ya tukio hilo gari hilo lilielekea barabara ya Geita mjini.
Majeruhi alifariki majira ya saa16:00 hrs wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya Geita.
Upelelezi wenye kuambatana na msako mkali unaemdelea kuwatafuta watuhumiwa

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More