Kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa hasa
kwenye mitandao ya kijamii zinazomuhusisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi aliyemaliza muda wake Ndg William Lukuvi kumpeleka
mfanyabiashara maarufu nchini Ndg Tanil Somaiya kwa Rais John Pombe
Magufuli ili kumtambulisha kwake mfanyabiashara huyo.
Taarifa
hiyo sio ya kweli, ni uzushi wa kutunga ambao unalenga kumchafua
Mheshimiwa Lukuvi na kuharibu haiba yake mbele ya jamii.
Tangu
baada ya kutangazwa, kuapishwa na kuanza kazi rasmi kwa Rais Magufuli,
Mhe Lukuvi hajawahi kwenda nyumbani kwake ama ofisini kwa lengo la
kumtambulisha mfanyabiashara wala mtu yeyote.
"Mimi
ni kiongozi wa muda mrefu mwenye uzoefu na ninayezingatia nidhamu ya
uongozi na utawala bora, siwezi kufanya jambo hilo ambalo ni kinyume na
kanuni, taratibu na sheria za kiutendaji" amesema Mheshimiwa Lukuvi.
Mhe
Lukuvi amesikitishwa sana na taarifa hiyo ambayo imeendelea kusambaa
mitandaoni na amewataka watanzania kuipuuza taarifa hiyo lakini pia
amechukua hatua stahiki zinazohusu makosa ya kimtandao kwa wanaohusika.
0 comments:
Post a Comment