WAKATI
Rais Magufuli akimpa heko Mbunge wa Kigoma Mjini Kupitia chama cha ACT
Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe kwa kitendo chake cha kutoungana na wabunge
wanaowakilisha umoja wa katiba ya wananchi Ukawa kupiga kelele na
kutolewa nje ya Bunge na Spika Job Ndugai,Zitto ameibuka na kuwaunga
mkono wabunge hao.
Akizungumza
nje ya bunge, muda mfupi mara baada ya bunge hilo kuhairishwa na Waziri
Mkuu Mhe Kasimu Majaliwa,Zitto alisema kuwa hakuna haja ya kuwajadili
wabunge hao kwa kuwa demokrasia inawapa haki ya kufanya hivyo.
Zitto
ambaye alikuwa akizungumza na Shirika la Habari Tanzania’TBC’ alisema
kuwa haoni sababua ya wabunge hao kuitwa wahuni au watoto kama
walivyoitwa Bungeni kwa kuwa kufanya hivyo ilikuwa ni sehemu ya
kuwasilisha hisia zao kwa walengwa.
Alisema
kuwa binafsi hana muda wa kulijadili suala hilo kwa kuwa limeshapita na
kinachotakiwa kwa sasa ni kufanya kazi iliyowapeleka bungeni.
0 comments:
Post a Comment