SHULE
ya Kimataifa ya Iringa imetoa wito kwa serikali ya Dk John Magufuli kuanzisha
mpango maalumu wa uingizaji na utumiaji wa teknolojia mbalimbali mpya kwa
maendeleo ya nchi kwa kutoa ufadhili wa elimu kwa makundi mbalimbali ya wanafunzi
watakaoplekwa katika nchi zenye teknolojia hizo.
Pamoja
na mpango huo, shule hiyo imeiomba serikali hiyo kutumia utajiri wa gesi ya
Mtwara kuendelea kuboresha mazingira na mifumo ya utoaji wa elimu nchini ili iwiane
na nchi zilizopiga hatua kubwa katika sekta hiyo.
Hayo
yalisemwa na mjumbe wa bodi ya shule hiyo, Edwin Porch kwenye maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya shule hiyo yenye wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari
zaidi ya 100, yaliyofanyika shuleni hapo juzi.
Mkuu
wa Utawala wa shule hiyo, Jean Milliken alisema; “Kwasababu shule yetu ni ya
kimataifa, tumekuwa na kawaida kila mwaka kuwa na siku hii, tunasheherekea
utaifa wetu kwasababu tunatoka mataifa mbalimbali.”
Milliken
alisema kwa kupitia siku hiyo; wafanyakazi, wanafunzi na wazazi na walezi wao hufanya
sherehe kwa kuonesha tamaduni za nchi wanazotoka vikiwemo vyakula vinavyoliwa
na mataifa hayo na kufanya maonesho mbalimbali yenye maudhui ya kukuza sekta ya
elimu nchini.
Akizungumzia
sekta ya elimu na matumizi ya teknolojia kwa maendeleo ya Taifa, Porch alisema;
“nchi inahitaji shule nyingi za vipaji maalumu sambamba na zile za kimataiafa
ili zitoe wataalamu wengi kwa faida ya nchi .”
Alisema
mazingira ya Tanzania yanaruhusu kufanyika kwa mapinduzi makubwa ya kiuchumi
kama uwekezaji wa kutosha utafanywa katika sekta ya elimu.
“Tanzania
inaweza kuwa kama Japan ambayo leo imepiga hatua kubwa ya maendeleo duniani
baada ya kuwapeleka watu wake katika nchi mbalimbali duniani ambako walijifunza
na kurudisha kwao tekenolojia zilizoliofanya taifa hilo liwe moja kati ya nchi
zilizoendelea kiviwanda,” alisema.
Alisema
wakati Japan ikipeleka watu wake katika nchi zingine zilizoendelea kujifunza
tekenolojia za huko haikuwa mzalishaji mkubwa wa magari lakini hivi sasa;
magari yake yanauzwa kila nchi duniani.
Alisema
Tanzania inaweza kuwa nchi ya viwanda vinavyotokana na matumizi ya tekenolojia
zake kama itathubutu kufanya kile kilichofanywa na Japan.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini, Salim Asas alisifia uwepo wa shule hiyo ya kimataiafa
mjini Iringa akisema unasaidia kuupaishia mkoa wa Iringa katika utoaji wa elimu
ya kimataifa.
Alisema
serikali ina kila sababu ya kuzisaidia shule za kimataifa ili zichukue
wanafunzi wengi zaidi wa kitanzania lakini pia zivutie wageni toka nje ya nchi.
Asas
alisema elimu inayotolewa katika shule za kimataifa ni elimu bora inayowaandaa
wanafunzi kushindana kimataifa katika nchi yoyote ile duniani jambo ni sifa na
ni maendeleo kwa nchi.
0 comments:
Post a Comment