Rais wa nchi ya kenya,Uhuru Kenyatta
Wakati wakenya wakiwa busy katika
kumtaka Rais wa Taifa hilo,Uhuru Kenyatta kufanya mageuzi makubwa katika
Serikali yake haswa katika suala la utekelezaji kama anavyofanya Rais
wa Tanzania Dr Magufuli,
Rais wa Kenya amefanya mabadiliko katika
Baraza lake la Mawaziri, na kuwafuta kazi mawaziri wote ambao wizara
zao zilizotajwa katika ufisadi.
Rais Uhuru Kenyatta amechukua hatua hiyo
siku moja tu baada ya kutangaza ufisadi kuwa tishio kwa usalama wa
kitaifa. Rais ameahidi kufanya mabadiliko zaidi katika afisi yake hivi
karibuni.
Katika hotuba ilioonyeshwa kwa njia ya
Televisheni,Rais Uhuru Kenyatta ameongeza idadi ya wizara kutoka kumi na
tisa hadi ishirini na kuongeza idara mpya chini ya wizara mbalimbali
katika kile alichosema ni kusaidia mawaziri kutekeleza majukumu yao bora
zaidi.
Idara hizo zimeongezwa kutoka ishirini na sita hadi arobaini na moja.
Rais Kenyatta amefanya mabadiliko katika
baraza lake la mawaziri baada ya mawaziri sita kulazimika kujiondoa
kutokana na wizara walizosimamia kuhusishwa na ufisadi huku wawili kati
yao wakikabiliwa na kesi mahakamani.
Ni Mabadiliko yaliyotarajiwa hasa baada
ya hatua ya aliyekuwa waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru kujihuzulu mwishoni
mwa juma kutokana na kile alichosema ni ushauri wa daktari wake- baada
ya usumbufu aliopata wizara yake ilipohusishwa na sakata kadhaa za
ufisadi.
Kwa mujibu wa katiba idadi ya mawaziri
inapaswa kuwa kati ya kumi na wanne na ishirini na wawili- na hivyo
kujiuzulu kwake kulisababisha idadi hiyo kupungua hadi kumi na tatu.
Baraza jipya la mawaziri linajumuisha wanawake wanne na wanaume kumi na sita.
Baadhi ya mawaziri wamesalia katika
nafasi zao huku wengine wapya wakiteuliwa kuchukua nafasi za mawaziri
waliohusishwa na ufisadi.
Hatua itakayofuata sasa ni kwa mawaziri wapya kuchunguzwa na kamati ya bunge kabla ya kuidhinishwa kikamilifu.
Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imekuwa
ikikabiliwa na changamo ya ufisadi katika wizara kadhaa na kumekuwepo
shinikizo sio tu kutoka kwa wananchi lakini pia kutoka kwa mashirika ya
kijamii,viongozi wa upinzani na hata mabalozi wa nchi za kigeni kutaka
hatua zichukuliwe.
0 comments:
Post a Comment