Vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umemteua, Goodluck Ole
Medeye (Chadema) kusimama katika nafasi ya uspika,huku katika nafasi ya
unaibu Spika akiteuliwa,Magdalena Sakaya wa Chama Cha Wananchi (CUF).
Tangu
kuanza kwa mchakato wa kumpata mwakilishi aliyekuwa anatazamiwa
kuwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika
kinyang’anyiro cha nafasi ya uspika Mpekuzi ilibaini kuwa jina la Goodluck Ole Medeye, ndilo lililokuwa likitajwa kuwa litasimamishwa katika nafasi hiyo.
Ole Medeye, aliwahi kuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi kupitia CCM,aliwahi
pia kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika
utawala wa awamu ya nne wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete (CCM).
Umoja wa Vyama unaofahamika kama Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.
0 comments:
Post a Comment