Jeshi la polisi mkoani iringa limewatahadharisha wananchi kuwa
makini ili kuepukana na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa iringa RPC RAMADHANI ATHUMANI MUNGI alipokuwa akizingumza na nuru fm juu ya kuzuia unyang’anyi wa kutumia silaha kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
hapohapo imeelezwa kuwa uelewa mdogo wa sheria katika jamii umetajwa kuwa
sababu ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa polisi mkoa wa
Iringa RPC RAMADHANI ATHUMANI MUNGI alipokuwa akizungumza na nuru fm mara baada
ya kutokea kwa tukio la wananchi kumuu mtu kwa kosa la kuiba spika ya redio.
Aidha ameitaja sababu nyingine ya wananchi
kujichukulia sheria mkononi ni pamoja na wananchi kutokuwa uhakika wa kujua mtu
wanaempiga ndiye muhusika.
Katika hatua nyingine kamanda mungi amewataka
wananchi kutoa taarifa katika jeshi la polisi na vyombo vya usalama wanapoona
matukio kama hayo ili kuendana na sheria ya nchi.
0 comments:
Post a Comment