BEN
SAANANE ambaye ni mkuu wa Idara ya sera na utafiti wa chadema
akionyesha baadhi ya picha za mauaji ya viongozi wa Chama hicho
yaliyowahi kufanyika na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hadi sasa
jambo ambalo sasa wamesema wamechoka na wameamua kujilinda wenyewe kwa
kuhakikisha kuwa wanawakamata wale wote walioendesha tukio la GEITA
Baraza la vijana la chama cha Demokocrasia na maendeleo chadema BAVICHA wametoa siku tatu kwa jeshi la polisi nchini kumwachia Mwenyekiti wa baraza hilo PATROBAS KATAMBI aliyekamatwa jana mkaoni mwanza pamoja na kuwakamata wahusika wote waliohusika na kifo cha Mwenyekiti cha CHADEMA mkoani GEITA Bwana ALPHONCE MAWAZO huku wakisema kuwa kama hayo hayatafanyika watalazimika kulipa kisasi.
Baraza la vijana la chama cha Demokocrasia na maendeleo chadema BAVICHA wametoa siku tatu kwa jeshi la polisi nchini kumwachia Mwenyekiti wa baraza hilo PATROBAS KATAMBI aliyekamatwa jana mkaoni mwanza pamoja na kuwakamata wahusika wote waliohusika na kifo cha Mwenyekiti cha CHADEMA mkoani GEITA Bwana ALPHONCE MAWAZO huku wakisema kuwa kama hayo hayatafanyika watalazimika kulipa kisasi.
Akizungumjza
na wanahabari mchana wa leo jijini Dar es salaam katibu wa uenezi wa
baraza hilo Taifa Bwana EDWARD SIMBEYE amesema kuwa kwa sasa vijana na
wanachama wa chadema wamechoka na mauaji ya viongozi wa chama hicho
huku kukiwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa wahusika hivyo sasa
wameamua kuhakikisha kuwa wanajilinda wenyewe ikiwa ni pamoja na
kuwatafuta wahusika wa tukio la Geita na kuwakamata kama polisi watakuwa
wameshindwa kufanya hivyo kwa muda muafaka..
Akizungumzia
tukio la jana mkoani mwanza amesema kuwa wakati jana mwili wa marehemu
MAWAZO ukiwasili katika hospitali ya BUGANDO kwa ajili ya kuhifadhiwa na
kufanyiwa uchunguzi zaidi Polisi walipanga njama za kuutorosha mwili wa
marehemu kwa ajili ya kwenda kuuzika kimya kimya jambo ambalo amesema
wanachama na viongozi wa CHADEMA walishtuka na kuamua kulinda mwili huo
na ndipo ilipotokea vurugu iliyopelekea kiongozi wa vijana taifa
kukamatwa na polisi .
Amesema
kuwa inashangaza kuona jeshi la polisi likiwa katika mstari wambele
kuhangaika juu ya mwili wa Marehemu ALPHONCE MAWAZO wakati iko wazi kuwa
wakati anauawa na wananchi polisi walikuwepo eneo la tukio na kushindwa
kutoa hata msaada wa gari kwa ajili ya kumpeleka hospitalini lakini
jana polisi walipata gari la kuja kumtorosha katika hospitali hiyo jambo
ambalo amesema limekuwa likifanywa na polisi kila mara yanapotokea
matukio ya mauaji kama haya.
Aidha
katika hatua nyingine vijana hao wametangaza rasmi kuwa baada ya siku
tatu na polisi kushindwa kuwaachia huru viongozi wao na kuwakamata
wauaji wa MAWAZO wamewaagiza vijana wote wa Tanzania kukusanyika kwa
wingi mkaoni mwanza kwa ajili ya kushinikiza kuwaachia viongozi wao
pamoja na kulinda mwili wa marehemu ALPHONCE MAWAZO ambao umelazwa
katika hospitali ya Bugando mkoani mwanza.
Marehemu
ALPHONCE MAWAZO aliuawa na wananchi mkoani GEITA baada ya kushambuliwa
na wananchi waliokuwa na sialaha za jadi ambao hadi sasa hakuna taarifa
rasmi inayoeleza hali halisi ya mauaji hayo.
0 comments:
Post a Comment