MWENYEKITI WA CHADEMA IRINGA MJINI FRANK NYALUSI
CHAMA cha Demokrasia na maendeleo chadema Jimbo la
Iringa mjini kimesema kesho/leo chama hicho kinaingia kwenye mchakato wa kura
za maoni za nani atakayekalia kiti cha
Meya na Naibu Meya ambaye ataongoza halmashauri ya manispaa ya Iringa kwa
kipindi cha mwaka 2015/2020.
Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Iringa ambaye pia ni diwani mteule
wa chadema kata ya Mivinjeni Frank Nyalus alisema kuwa hadi sasa
wameshajitokeza madiwani watatu sita ambao watatu wameingia kwenye kinyang’anyiro
cha Meya na wengine watatu kwenye kinyang’anyiro cha Unaibu Meya.
Nyalusi aliwataja madiwani ambao wemejitokeza kuchukua fomu
ya kugombea nafasi hizo huku wakisubiria maamuzi ya chama hicho.
Waliojitokeza kuwania nafasi ya Meya ni Diwani wa kata
ya Mivinjeni Frank Nyalus,diwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata na Diwani wa
kata ya Isakalilo Alex Kimbe.
Waliojitokeza kuusaka unaibu Meya ni diwani wa kata ya
Gangilonga Dadi Igogo,Diwani wa kata ya Kwakilosa Joseph Lyata na diwani wa
kata ya mkimbizi Evaristo Mtitu.
Mchakato wa uchukuaji wa fomu ulianza Novemba 21 Mwaka huu na wanatarajia kurudisha
fomu hizo leo Novemba 24 na kuingia kwenye kura za maoni huku gharama ya fomu zikiwa Tsh.50,000
kwa kila moja.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa manispaa ya Iringa wakiwamo
madiwani wenyewe wamekuwa na mchecheto wa kumjua nani atakaye kuwa mrithi wa Meya
aliyemaliza muda wake na pia ni diwani mteule wa chama cha mapinduzi (CCM) kata
ya Mlandege Aman Mwamwindi.
Akizungumza mmoja wa wafanyabiashara wa wadogo mjini
Iringa Pendo Yugin alisema kuwa wao wanawataka madiwania hao kumchagua meya
atakayetokana na wao ambaye atawatetea hata kwenye biashara zao badala ya
kuwanyanyasa.
Aidha waliogombea nafasi ya Meya wameliambia Nipashe
kwamba lengo lao la kugombea ni kuifanya
manispaa hiyo iwe ya mfano kwenye miradi ya maendeleo tofauti na kipindi cha
meya aliyemaliza muda wake.
0 comments:
Post a Comment