Monday, June 20, 2016

MIRADI 43 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSH BILIONI 23 KUZINDULIA NA MWENGE MKOA IRINGA

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Bi Amina Masenza  (kushoto)  akikabidhiwa  mwenge  wa Uhuru  na  mkuu  wa  mkoa  wa  Njombe baada  kuwasili mkoa  wa  Iringa  ukitokea  mkoa  wa  Njombe zaidi ya  miradi 43  yenye  thamani  ya  zaidi  ya  Tsh bilioni 23 kuwekea mawe  ya  msingi na  kuzinduliwa
Mkuu  wa mkoa   wa  Iringa Bi  Amina  Masenza  akicheza pamoja na  wakuu  wake  wa  wilaya za  mkoa wa Iringa  kabla ya  kupokea mwenge 
MWENGE  wa  uhuru  waanza  mbio  zake  mkoani  Iringa  leo kwa  kuzindua na  kuweka mawe ya  msingi katika   miradi ya  kimaendeleo  43 yenye  thamani ya  zaidi  ya Tsh  bilioni 25 .4 
Huku    kiongozi  wa  mbio  za  mwenge  kitaifa George Mbijima akiwashukia  baadhi  ya   watu wanaopinga  mbio  hizo  za  mwenge  wa  Uhuru  kuwa  hawapo  sawa na  wanapaswa kupelekwa  milembe kuchunguzwa  utashi wao. Akipokea  mwenge  wa  uhuru kutoka  mkoa  wa  Njombe  jana mkuu  wa mkoa  wa Iringa Bi Amina  Masenza  alisema  kuwa   ujumbe  wa mbio  za mwenge wa Uhuru  ni Vijana nguvu kazi yua taifa  washirikishwe  na  wawezeshwe .
Mkuu  huyo  wa  mkoa  alisema  kuwa  uwezeshaji  wa  vijana  kushiriki  katika maendeleo ya  mkoa  huo umekuwa  ukipewa  kipaumbele  zaidi  ikiwa  ni pamoja na  kutafuta  ufumbuzi wa  changamoto mbali mbali  zinazokwamisha  vijana  kujiajiri  na kuajiriwa ndani ya mkoa na taifa .

“ mkoa  umekuwa  ukitekeleza  mikakati  mbali mbali  ikiwemo ya  kutenga maeneo   kwa  ajili ya  vijana na mfano Mufindi  imetenga  maeneo  kwa ajili ya vijana  ardhi  yenye  ukumbwa wa  hekta 870, Iringa Hekta 79 ,Kilolo Hekta 192 na Iringa Manispaa imetenga  maeneo 12 huku  mji Mafinga eneo moja “

Alisema  lengo la kufanya  hivyo ni kuwaunganisha  vijana  na taasisi  za kifedha  kwa  ajili ya  kupata mikopo  yenye  riba ndogo   na masharti nafuu  pia  kushirikiana na wadau  wa maendeleo  ya  vijana katika kutoa elimu ya  ujasiliamali  ,stadi  za kazi na  stadi  za maisha 

Pia  kutoa  mikopo  yenye  thamani ya  zaidi ya  Tsh 942,952 ,622 kwa  vijana  asilimia  tano  waliopo mkoani hapa  kupitia  fedha  za  makusanyo  ya ndani kwenye  halmashauri  ambazo  ni  fedha zilizotengwa kwa  mwaka  wa fedha  2016 na  2017.

Hata  hivyo  alisema mkoa  umejipanga na  tayari  umeanzisha  skim  za  umwagiliaji  ili  kufanya  kilimo chenye tija na kuwawezesha  vijana  kujiajiri  kupitia  kilimo kisichotegemea  mvua .

Akizungumzia  juu ya mapambano  dhidi ya  rushwa alisema  kuwa kwa mwaka 2015 /2016 mkoa  umetoa elimu  ya   mapambano ya Rushwa  kwa wananchi 22,402 wakiwemo  wanafunzi 11,838 na kuendesha semina 101 na mikutano 53 na  kuwa  jumla ya  taarifa 132 zimepokelewa  kati  ya mwaka 2015 na 2016 huku taarifa 41 zilifunguliwa  majalada  kwa  ajili ya uchunguzi wa taarifa  za  rushwa  na kesi 21 ziliweza kufunguliwa Mahakamani  ambapo  kesi  6 zilitolewa  hukumu .

Aidha mkuu  huyo wa mkoa  alisema kuwa mkoa  wa  Iringa umeendelea na jitihada za  kupunguza makosa yatokanayo na madawa ya kulevya  kwa asilimia 32.72 kwa  kipindi cha mwaka mmoja  uliopita  kwa kutoka  asilimia 89 kwa mwezi janjuari  hadi Mei 2015 kwa kufikia  49 kwa  kipindi cha januari hadi  Mei 2016 huku  kiwango  cha  dawa  za  kulevya  kimepungua  kutoka  kilo 506.5  kwa  Januari  hadi Mei 2015 hadi kufikia kilo 13.9  kwa januari  hadi mei 2016.

Kwa  upande  wake  Kiongozi  wa  mbio  za  Mwenge  Kitaifa  Bw Mbijima  aliwapongeza  wananchi wa mkoa wa  Iringa  kwa  kuchangia  mkiradi ya  Mwenge  kwani  alisema  kuwa  miradi   hiyo ni fahari  kwa mkoa na Taifa  katika  kuwakomboa  wananchi  wa  mkoa  huo.

Bw Mbijima  alisema  kuwa  wapo  baadhi ya  watu ambao  wamekuwa  wakihamasisha  jamii kuchukia mwenge  wa Uhuru jambo  ambalo ni ukosefu wa  uzalendo  kwa  Taifa  na  kuwa baadhi ya  nchi ulimwenguni  zimekuwa  zikitamani  kuiga  kukimbiza  mwenge  lakini  zinashindwa  .

Alisema  Tanzania  imekuwa ni mfano   kwa mataifa  mengine  katika  ukimbizaji  wa mwenge  wa uhuru na baadhi ya  nchi zimeishika njiani katika  kukimbiza  mwenge  wa  uhuru hivyo  kuwataka  wananchi  kuendelea   kupenda  mwenge  wa  Uhuru na kuwapuuza  wanaobeza  mwenge  wa  uhuru na kuwataka wapelekwe  milembe  ambako ni  Hospitali ya vichaa  kuchunguzwa akili  zao.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More