Thursday, June 2, 2016

Wabunge Wote Wa Upinzani Watoka Nje Asubuhi Hii Kupinga Naibu Spika Kuendesha Vikao vya Bunge

Wabunge wote wa vyama vya upinzani leo tena  wametoka nje kupinga Naibu Spika wa Bunge  Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.

Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge, wabunge hao wametoka nje  majira ya saa 3:00 asubuhi na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More