Thursday, June 30, 2016

MKOA WA IRINGA WAKAMILISHA MADAWATI YA MAGUFULI

 SERIKALI    ya    mkoa wa  Iringa  imetekeleza  agizo la  Rais  Dr  John Magufuli  kwa kukabidhi  jumla ya madawati 21,304 kwa   shule  za  msingi na   sekondari katika Halmashauri  zote  tano  za  mkoa   huo .

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Bi  Amina  Masenza  akikabidhi  mgao wa madawati hayo kwa  wakurugenzi wa Halmashauri   hizo leo  zoezi lililofanyika kwenye  karakana na  chuo  cha  ufundi  stadi  VETA , alisema kuwa  utekelezaji  wa  agizo  hilo  umefanikiwa  kutokana na  mwitikio mzuri wa  wananchi  wa  mkoa  huo  na  wadau mbali  mbali wa  maendeleo ambao  kwa  umoja  wao wamesaidia zoezi hilo  kukamilika .

 Alisema  kuwa Rais Dr  Magufuli  alitoa  agizo kwa  wakuu  wote wa  mikoa nchini kuhakikisha  wanafunzi wote wanakaa katika madawati  ifikapo leo Juni 30  mwaka  huu na    kutokana na agizo hilo alilazimika kuwashirikisha   wakuu  wake  wa  wilaya  na  wadau mbali  mbali wakiwemo  wananchi  mmoja  mmoja na  kila  mmoja kwa  uwezo  wake aliweza  kuchangia madawati hadi  kufanikisha  zoezi hilo.

Mkuu  huyo  alisema kwa Halmashauri za  mkoa wa  Iringa zimetengeneza madawati  kupitia  bajeti  zake  na  wadau  waliopo kwenye  Halmashauri  husika  na    hadi sasa  mkoa   umeweza  kutengeneza madawati hayo 21,304 wakati     madawati  8,163 kwa  ajili ya  shule za msingi  huku madawati 1,264  ya  shule za  sekondari  yanaendelea  kutengenezwa  katika karakana mbali mbali   na  fedha  kwa  ajili ya matengenezo hayo  tayari  zimelipwa .

 Hivyo  alisema  madawati  yanayoendelea kutengenezwa  yanatarajiwa  kukamilika July 15 mwaka  huu kwani  yamechelewa  kukamilika  kutokana na  wakandarasi wanaotumika  kutengeneza  madawati  hayo  kuwa na kazi nyingi .

Bi Masenza  alisema  kuwa  ofisi  yake  kwa  kushirikiana na  wadau  mbali mbali imeweza kutengeneza  madawati 700 kwa  lengo la  kuunga mkono jitihada za  Halmashauri za kumaliza tatizo  la  madawati mapema ,ambayo yamegawiwa  katika Halmashauri tano za  mkoa wa  Iringa ambazo ni Iringa Manispaa madawati 200, Mji Mafinga  madawati 100 ,Halmashauri ya Iringa madawati 100 ,halmashaur i ya  Mufindi madawati 100 na  Kilolo madawati 100

 “Nitumie fursa hii kuwashukuru wadau mbalimbali,wafanyakazi  wa Halmashauri na wananchi wote walioona umuhimu wa kuchangia upatikanaji wa madawati haya”alisema Masenza na kuongeza.

 “Mchango wao umekuwa na umuhimu katika kuwaandaa vijana wetu tunapoelekea Taifa lauchumi wa kati ifikapo mwaka 2030,michango yao ndiyo iliyosababisha kuwapo kwa ziada hiyo,kwani mkoa umetoa madawati 200 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na madawati 100 kwa Halmashauri za Kilolo,Iringa,Mji Mafinga na Mufindi”alisema Masenza.

 Wakati  madawati  308 yanaendelea   kutengenezwa  katika karakana ya VETA  pindi yatakapokamilika  yatafikisha idadi ya madawati 1,008  jumla ya fedha  ambazo zimetumika  kutengeneza  madawati  hayo 1,008 ni milioni 50,400,000 na  baada ya madawati  yote  kukamilika   kutengenezwa mkoa  wa Iringa hautakuwa na  upungufu wa madawati  kwa  wanafunzi  zaidi ya  kuwa na ziada ya madawati .

“Kazi ya kutengeneza madawati itakapokamilika Shule za Mkoa wa Iringa hazitakuwa na upungufutena wa madawqati bali zitakuwa na ziadiyamadawati 850 na hiini kutokana na baadhi ya Halkmashauri kuwa kutengeneza madawati ya zaidi na mengine niyaleyaliyotolewakutoka Ofisi ya Mkoawa Iringa”alisema Masenza.

Mkoa  wa  Iringa  una jumla ya   shule  za msingi 478 na  shule za  sekondari 107zinazomilikiwa na  serikali  na  mkoa  huo  ulikuwa na  upungufu wa madawati 29,347  ikiwa ni madawati 26,046 ya  shule  za Msingi na madawati 3301 kwa  shule za  sekondari.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More