WATANZANIA wametakiwa kuingia katika ubia kama wajasiriamali badala ya kufikiria kwamba wao ni maskini na hawana fedha za kuingia ubia na makampuni ya nje.
kauli hiyo imetolewa katika wiki ya Ufaransa ambapo makampuni 50 yanashiriki kuonesha uwezo wa utayari wa ushiriki wao katika ujenzi wa uchumi wa kati wa Tanzania unaotegemea viwanda.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi ambaye aliwasilisha haja na matamanio ya Watanzania kwenye sekta binafsi katika kushirikiana na wawekezaji kutoka Ufaransa, alisema watanzania wamekuwa waoga kuomba ubia wakidhani kwamba hawana kitu cha kutoa wakati wao wana akili na rasilimali.
[caption id="attachment_1654" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi akizungumza katika kilele cha wiki ya Ufaransa ambapo wawekezaji kutoka makampuni 50 ya Ufaransa walishiriki katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliombatana na maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wafaransa. (Picha zote Thebeauty.co.tz)[/caption]
Kauli hiyo ambayo aliisema kwenye mazungumzo na wawekezaji hao wa Ufaransa wakati akielezea utayari wa sekta binafsi kushirikiana na Wafaransa alisema kwamba watanzania wengi hawajiamini na kwamba wakati umefika kwa Watanzania kujitambua kwa kuwa wao (wafaransa) walijaribu wakaweza kwani kama sisi walikuwa na vitu vya ziada katika uthubutu wao.
Katika mazungumzo yake Dk. Mengi akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye alisema kwamba sekta binafsi ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi inawezekana kwa watanzania kuthubutu.
Aidha alisema uwapo wa Wafaransa utaweza kusaidia kupandisha uwezo, teknolojia na utaalamu hali ambayo inawezekana kupitia uwapo wa shughuli za ubia kati ya wawekezaji wa Kitanzania na Wafaransa.
[caption id="attachment_1655" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye (kulia) akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.[/caption]
Alisema baada ya sekta ya umma kuweka miundombinu mahala pake, ni kazi ya sekta binafsi kutumia miundombinu hiyo kubuni na kuwekeza katika viwanda na kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Dk.Mengi alisema kwamba TPSF inaamini kwamba sekta binafsi ni ufunguo katika kuongoza na kuimarisha uchumi wa Tanzania ambao unatakiwa kuwa endelevu kama awamu ya tano inavyotaka.
Aliwaambia wafanyabiashara wa Ufaransa kwamba Tanzania ina kila kitu wanachohitaji na kwamba makampuni makubwa ya Ufaransa kama Airbus, Renault, Alstrom, Systra wana mtandao mpana duniani wa kufanyabiashara na wawawekezaji wadogo duniani hivyo wanaweza kufanya hivyo hapa nchini.
[caption id="attachment_1656" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.[/caption]
Alisema changamoto za utaalamu zitaondoka kwa ushirikiano na uwezeshaji.
Aliwataka wawekezaji hao wa Kifaransa kwamba Tanzania kwa sasa ndio nchi ya uwekezaji na kusema changamoto zilizopo ni fursa za uwekezaji nchini Tanzania hasa katika nishati ambapo taifa hili litahitaji megawati 10,000 ifikapo mwaka 2040.
Aidha alisema anaamini kwamba wengi wa watanzania wapo tayari kushirikiana na Ufaransa katika kuhakikisha kwamba wanaingia ubia katika biashara halali na yenye kusaidia pande zote.
Naye Simbeye alisema anatamani kuona kwamba wafaransa wanawekeza kiwanda cha magari nchini kwani inawezekana kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo wa uwekezaji kwa sasa.
[caption id="attachment_1659" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo katika mkutano huo kwenye kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.[/caption]
[caption id="attachment_1660" align="aligncenter" width="1404"] Mmoja kati ya wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa akiuliza swali kwa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) katika kilele cha mkutano wa wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.[/caption]
[caption id="attachment_1661" align="aligncenter" width="1404"] Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi, Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira katika mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa.[/caption]
[caption id="attachment_1662" align="aligncenter" width="1404"] Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa pili kulia) pamoja na baadhi ya viongozi wa wizara walioshiriki mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.[/caption]
[caption id="attachment_1663" align="aligncenter" width="1404"] Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara katika Ubalozi wa Ufaransa nchini, Blevin Claude (wa pili kushoto) akiwa na Ofisa anayeshughulikia masuala ya Uchumi katika Ubalozi wa Ufaransa nchini, Beatrice ALPERTE (kushoto) katika mkutano huo.[/caption]
[caption id="attachment_1664" align="aligncenter" width="1404"] Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua masomo ya biashara walioshiriki mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa uliofanyika katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.[/caption]
[caption id="attachment_1666" align="aligncenter" width="1404"] Sehemu ya wadau na wafanyabiashara kutoka makampuni 50 ya nchini Ufaransa walioshiriki mkutano huo.[/caption]
[caption id="attachment_1667" align="aligncenter" width="1404"] Mkutano ukiendelea.[/caption]
[caption id="attachment_1668" align="aligncenter" width="1404"] Sales Executive wa kampuni ya CMC Formula wauzaji wa magari ya Renault, Erica George akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi wakati akitembelea mabanda katika maadhimisho ya wiki ya Ufaransa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.[/caption]
[caption id="attachment_1669" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi akipata maelezo katika banda la kampuni ya TOTAL.[/caption]
[caption id="attachment_1670" align="aligncenter" width="1404"] Meneja Mauzo wa Kampuni ya AIRBUS HELICOPTERS, Jean-Marc Royer (kulia), akitoa maelezo ya shughulli wanazofanya kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (wa pili kushoto) alipotembelea mabanda ya kampuni mbalimbali kutoka nchini Ufarasan zilizoshiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya Ufaransa yaliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam Kushoto ni Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara Ubalozi wa Ufaransa, Blevin Claude.[/caption]
[caption id="attachment_1674" align="aligncenter" width="1404"] Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara Ubalozi wa Ufaransa, Blevin Claude akitoa neno la shukrani kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi wakati Dk. Mengi akijiandaa kuondoka katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa yalipofanyika maadhimisho ya wiki ya Ufaransa jijini Dar es Salaam.[/caption]
0 comments:
Post a Comment