Na Fredy Mgunda, Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kuwachukulia hatua watu wote waliohusika na uharibifu wa mlima uliopo Kata ya kitanzini miomboni kutokana na mlima huo kuwa ni hifadhi ya taifa.
Akizungumza na blog hii Kasesela alisema kuwa amesikitishwa na wananchi walivamia mlima huo na kuanza kujenga vibanda wakati kuna maeneo mengi yapo hapa Manispaa hivyo ni lazima hatua zichukuliwe kwa sababu saizi tunahangaika kutunza uoto wa asili halafu watu wengine wanaharibu.
"Nimefika katika eneo lile kweli wananchi wamevamia bila hata mimi kiongozi wa wilaya sijui nafikiri wametumia fursa ya sikukuu hii ya pasaka kufanya uharibu huo sitakubali kuona nakiuka maagizo ya Makamu wa Rais ya kutunza uoto wetu wa asili"alisema Kasesela
Kasesela amemuagiza Mkurugenzi kulifiatilia swala hilo na kukikisha inapofika kesho saa nne Vibanda vyote viwe vimevunjwa na kuanza kupanda miti maeneo yote yaliyokatwa miti na kuhakikisha eneo liloharibiwa linarudi kwenye ubora wake.
"Kufikia kesho saa nne vibanda vitakuwa vimebomolewa hatuwezi kuaharibu eneo kama lile lazima wachukuliwe hatua kuanzia wananchi hadi viongozi waliohusika na mpango huo kwa kuwa wananchi hawawezi kuanza wenyewe bila kupata ruhusa kutoka kwa viongozi furani" alisema Kasesela
Lakini Kasesela alisema kuwa atakikisha anawachukulia hatua viongozi wenye uelewa mdogo wa namna ile kwasababu kiongozi mwenye akili na uelewa mkubwa hawezi kuruhusu kuaharibiwa eneo hilo.
Nawaomba wananchi wa Manispaa ya Iringa na Wilaya yote ya Iringa kuwa makini wanapoambiwa kufanya biashara katika mazingira yaliyohifadhiwa kwa kuwa wanaharibu mazingira makusudi na pia wanapata hasara zisizo kuwa na maana mfano walivamia huo mlima tayari wameshapata hasara lakini wameipa hasara kubwa serikali na jamii yote.
Uharibifu mkubwa unaofanywa katika mlima huo ukifumbiwa macho kama ilivyo ni wazi uongozi wa Manispaa ya Iringa umepuuza agizo hilo la makamu wa Rais na uwezekano wa uhifadhi wa ikolojia ya mto Ruaha kwa mwendo huo itakuwa ni ndoto ya alinacha
Uharibifu mkubwa unaofanywa katika mlima huo ukifumbiwa macho kama ilivyo ni wazi uongozi wa Manispaa ya Iringa umepuuza agizo hilo la makamu wa Rais na uwezekano wa uhifadhi wa ikolojia ya mto Ruaha kwa mwendo huo itakuwa ni ndoto ya alinacha
0 comments:
Post a Comment