Tuesday, April 18, 2017

KIMENUKA: Trump Aamuru Ndege za Kivita Zianze Kuruka Kuelekea Korea Kaskazini

Ndege hatari na mpya zilizotengenezewa kwa teknolojia ya hali ya juu za F-35 Stealth Fighter Jets tayari zimeruka kutoka jimbo la Utah lililopo magharibi mwa nchi ya Marekani na kutua UK tayari kabisa kwa training ya mwisho kuelekea uwanja wa vita.
Ndege hizi ambazo ni mpya na toleo la mwisho limemalizika kutengenezwa na kujaribiwa March mwaka huu 2017 zinatajwa kuwa ndege hatari zaidi katika Ground Attacks na Air Defence Missions. Zimepelekwa nchini Uingereza kwa training ya mwisho kuingia vitani ikiwa na malengo mawili, moja zitabaki bara la ulaya kulinda uvamizi wa Urusi na pili kupelekwa uwanja wa vita huko Norh Korea.
Wakati huohuo makamu wa rais wa marekani bwana Mike Pence Leo asubuh ametembelea ngome (base) ya marekani huko Korea ya kusini ya Camp Bonifas ambayo iko mpakani kabisa mwa North Korea na South Korea eneo lenye tension kubwa zaidi na hofu.
Pence amewatoa hofu wananchi wa South Korea kuwa USA iko tayari kuwalinda na madhara ya vita inayokwenda kutoka muda sio mrefu kwa hiyo wasihofu kabisa kuhusu usalama wao. Bwana Pence amesema Kim aache kutest makombora Mara moja na badala yake ayaingize uwanja wa vita kabisa kuliko mbwembwe za majaribio yasiyofanikiwa. Mike Pence ameziomba jumuia za kimataifa kuungana na Marekani kuuangamiza kabisa utawala wa Pyongyang chini ya Dikteta Kim. Hotuba hii ya leo ya Makamu wa Rais bwana Pence huko Camp Bonifas, South Korea inaonyesha dhahiri kuwa ni wazi Marekani inakwenda kuivamia kijeshi North Korea muda wowote kuanzia leo
Source: CNN na NBC News

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More