KAMATI iliyoteuliwa na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kusimamia uchaguzi wa klabu ya Lipuli Fc ya mkoani Iringa kuanza kutoa fomu kwa wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya Klabu hiyo ya Lipuli Fc kesho jumamosi Aprili 22 huku ikionya mwanachama atakayekiuka taratibu atafutwa kwa kugombea .
Akizungumza na wanahabari leo katika uwanja wa samora ,mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo Hamimu Mahmud Omary alisema kuwa kamati yake inaundwa na wajumbe watatu ambao wameteuliwa na TFF taifa kwa ajili ya kumaliza mgogoro huo wa Lipuli Fc pamoja na kufanya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo .
Hivyo alisema kwa ajili ya kuondoa figisu figisu katika uchaguzi huo wameteuliwa watu huru ambao wataanza zoezi hilo la utoaji wa fomu kwa wale ambao wanasifa ya kugombea nafasi zilizotanganzwa katika klabu hiyo ya Lipuli Fc na kuwa wanachama zaidi ya 1000 ndio ambao watashiriki kupiga kura na kuomba uongozi .
Mwenyekiti huyo alisema kwa wanachama wote wenye sifa watatakiwa kufika kulipia ada ya uanachama wao na kuwa mwanachama asiye hai hataruhusiwa kugombea au kuchagua viongozi .
" Orodha iliyofanyiwa uhakiki na kamati hii kama maagizo ya TFF yanavyosema ndio itatumika kujua nani ana siafa ya kushiriki uchaguzi huo na nani harusiwi na orodha hiyo itatandikwa eneo la wazi ili kila mwanachama aweze kuisoma na kuhakiki ....wanachama wanapewa siku saba kuanzia leo kufika kuhakiki kadi zao "
Akisoma kalenda hiyo ya uchaguzi wa Lipuli Fc alisema kuanzia Aprili 21-28 /2017 kwa maana ya jana ni kamati ya TFF kutangaza uchaguzi huo wakati Aprili 22 pazia la uchukuaji fomu kwa wanachama wote wenye sifa linafunguliwa wakati Aprili 29-30 kamati yake itabandika orodha ya awali ya wagombea kwenye mbao za matangazo na kipindi cha kupokea pingamizi ni Mei 1-2 mwaka huu .
Mwenyekiti huyo alisema mei 6 ni siku ya kamati yake kutangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo pingamizi na kufanya usahili wa wagombea baada ya hapo Mei 4-7 ni siku ya kamati yake kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye kamati ya maadili ya TFF huku Mei 7-11 ni kipindi cha kupokea ,kusikiliza na kutolea maamuzi masuala ya maadili kazi itakayofanywa na TFF Mei 12 kutangaza maamuzi ya kamati ya maadili .
Hata hivyo alitangaza kipindi cha kukata rufaa kamati ya uchaguzi ya TFF kwenye kamati ya rufaa ya uchaguzi kuwa ni mei 13-14 wakati rufaa hizo zitasikilizwa na kamati husika Mei 15-19 mwaka huu na Mei 20 wagombea wote kujulishwa na kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF na Mei 21 kuchapisha orodha ya mwisho ya wagombea na kutangazwa kwenye mbao za mataangazo .
Kuhusu kipindi cha kampeni kwa wagombea alisema muda ni kuanzia Mei 22-28 mwaka huu na atakayefanya kampeni kabla ya muda huo au kutoa rushwa ya aina yeyote atakuwa amepoteza sifa ya kuwa mgombea na kuwa uchaguzi wa Klabu ya Lipuli Fc utafanyika siku ya Mei 29 mwaka huu wajumbea na wagombea wote watapaswa kushiriki .
Mwenyekiti huyo alitaja nafasi zinazogombea na gharama ya fomu kwenye mabano kuwa ni mwenyekiti (200,000), makamu mwenyekiti (200,000) katibu na makamu wake (200,000),mweka hazina na msaidizi wake 100,000 na wajumbe watano wa kamati ya utendaji (100,000)
Alisema kuwa lengo la kutoa muda zaidi wa uchukuaji wa fomu ni kutaka kutoa nafasi kwa wanachama waliopo nje ya nchi nao kushiriki kugombea ama kuchagua na kuwa uongozi mpya wa Lipuli Fc utakabidhiwa pesa ya ada ya wanachama na idadi kamili ya wanachama baada ya uchaguzi huo .
Aidha mwenyekiti huyo alionya wagombea ambao wataanza kampeni za kuchafua watu wakiwemo viongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa ama viongozi wa TFF wilaya , mkoa hadi Taifa kuwa watakuwa wamepoteza sifa na hatua za kisheria dhidi yao zitachukuliwa .
Pia alisema sifa 7 ambazo mgombea anapaswa kuwa nazo ili kuwa mgombea wa Lipuli FC kuwa ni awe raia wa Tanzania , awe amesoma hadi kidato cha nne na kufuaulu au elimu ya juu ,awe na uzoefu wa angalau wa miaka 5 katika mambo ya utawala wa michezo ya mpira wa miguu,awe hajawahi kukutwa na hatia ya kosa la jinai na kuhukumiwa kufungwa bila kutolewa adhabu ya faini , awe na umri usiopungua miaka 25,awe na uwezo ,heshima, uadilifu, na haiba ya kuweza kuiwakilisha klabu ya Lipuli Fc ndani na nje ya mkoa wa Iringa na Tanzania ,asiwe na mwamuzi wa mpira wa miguu anayefanya shughuli za uamuzi kwa kipindi hiki.
0 comments:
Post a Comment