SERIKALI imeipongeza familia ya
mfanyabiashara Ahamed Huwel kwa kuitikia wito wa Rais John Magufuli wa kuifanya
Tanzania nchi ya viwanda kwa kuanzisha kiwanda cha kisasa cha maji mjini Iringa
yanayojulikana kwa jina la Maji Mkwawa.
Maji hayo yaliyoingizwa sokoni
hivikaribuni yalizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa
uzinduzi wa mashindano ya magari Iringa yaliyodhaminiwa na kiwanda hicho, wiki
iliyopita.
Akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa
washindi wa shindano hilo la magari Mkuu wa Mkoa alisema; “Uzalendo ni pamoja
na kujivunia kile tunachozalisha.”
Alisema Ahamed Huwel ametekeleza kwa
vitendo kauli ya Rais Dk Magufuli ya Tanzania ya Viwanda kwa kuanzisha kiwanda
hicho cha kisasa, kilichobaki ni kwa wadu kumuunga mkono.
“Kazi imebaki kwetu wana Iringa, ni
muhimu tukamuunga mkono kwa kuwa wa kwanza kuyatumia maji haya,” alisema huku
akiyapigia debe maji hayo kwa watanzania wengine.
Masenza alisema mbali na kiwanda hicho
kuchangia pato la Taifa, kinatarajia pia kutoa ajira za moja kwa moja kiwandani
na zile za mtu mmoja mmoja, kampuni au taasisi zitakazokuwa zikifanya biashara
ya maji hayo.
Msimamizi wa Uzalishaji wa kiwanda hicho,
Kevin Robert alisema kiwanda hicho ambacho mpaka sasa kimekwisha ajili
wafanyakazi 23 wa kudumu kina uwezo wa kuzalisha lita 28,000 kwa saa.
“Na kitakuwa kifanya kazi kwa saa nane
kila siku hivyo kuzalisha lita 224,000 kwa siku zitakazojazwa kwenye chupa za
ujazo tofauti kwa kuzingatia mahitaji na kipato cha mtu,” alisema.
Alisema Maji Mkwawa yataingia sokoni
wakati wowote kuanzia sasa baada ya kiwanda hicho kukamilisha taratibu chache
za uzalishaji zilizasalia.
Akizungumzia tofauti ya maji hayo na ya
viwanda vingine, Robert alisema; “Maji Mkwawa ni salama kwasababu yanatoka
chini ya ardhi na yanazalishwa kwa kutumia tekenolojia ya kisasa.”
0 comments:
Post a Comment