mwenyekiti
wa kijiji cha Ihefu kilichopo kata ya Mdabulo wilayani Mufindi Bateli Basilu akizungumza wa mwandishi juu tatizo lilopelekea kutoitisha mkutano wa mapato na matumizi kwa takriba miaka mitatu kutokana na utata wa fedha za wananchi milioni irishini na tano.
Na Fredy Mgunda,Iringa
Wananchi wa kijiji cha Ihefu
kilichopo kata ya Mdabulo wilayani Mufindi wameulalamikia uongozi wa kijiji kwa
kutowasomea mapato na matumizi kwa takribani miaka mitatu bila kuwaambia
chochote kinachoendelea ndani ya kijiji hicho.
Wakizungumza na blog hii
wananchi wa kijiji hicho walisema kuwa uongozi wa kijiji umekuwa unamatumizi yasiyo sahihi kwa rasilimali za
kijiji hadi kupelekea upotevu wa zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano
ambazo hazijulikani wapi zilikopotela.
“Viongozi wetu si waadilifu
wala si wawajibikaji kwa kuwa hawana uwezo wa kutuongoza haiwezekani zaidi ya
miaka mitatu hatuna mkutano wa hadhara wala hatusomewi mapato na matumizi je
hiki kijiji hakina mipango yoyote endelevu kwa kuwa wananchi hatujui nani
anaiongoza serikali hii” walisema wananchi
Wananchi waliongoza kuwa
mtendaji na mwenyekiti hawapatani hivyo hatuwezi kupata jibu wapi pesa zetu
zimeenda kutoka na viongozi hawa kutokuwa waadilifu na sio wawajibikaji kwa
wananchi.
“Hiki ni kijiji lazima kiwe
na mipangilio ya kuleta maendeleo lakini hapa tumekuwa mabubu maana hatujui
hata nini serikali yetu inamikakati gani ya kimaedeleo na saizi wananchi
tumeamka hatupo tena usingizini tunaomba mkutano uitwishe na kujua kwa miaka
yote mitatu kijiji kimefanya nini na vipi kuhusu upotevu wa pesa za wananchi”
walisema wananchi.
Aidha wananchi hao walisema
kuwa wamekuwa wakiishirikisha serikali ya kata chini mtendaji wa kata pamoja na
diwani wa kata lakini kila siku wanadanganywa tu hivyo wanauomba uongozi wa
wilaya au mkoa kusaidia kutatua tatizo la kuwa na viongozi ambao ni wabadhilifu
wa mali za wananchi.
Kwa upande wake mwenyekiti
wa kijiji cha Ihefu Bateli Basilu alikili kuwepo kwa upotevu wa pesa za
wananchi ambazo ni zaidi ya milioni mbili na sio milioni ishirini na tano kama
wanavyosema wananchi.
“Kweli mtengaji wetu alikula
fedha za wananchi na ndio kitu kilichosababisha wananchi kukataa kufanya
maendeleo ya kijiji wakitaka majibu sahihi ya hizo fedha zilipo”alisema Basilu
Basili alisema kuwa anapata
shida kukiongoza kijiji hicho kutokana na sitofahamu inayoendelea kijijini hapo
lakini aongeza kuwa mtendaji huyo sio muadilifu kabisa saizi hakuna maendeleo
yoyote yanayoendelea katika kijiji hicho.
“Ni kweli hili ni tatizo
kubwa sana hapa kijijini maana hadi mimi mwenyewe najifikiria kujiudhuru
kutokana sakata hili maana nimenichafua na kunialibia dira ya mipango yangu ya
kukipa maendeleo kijiji na wananchi wangu naomba uongozi wa juu kulitafutia
ufumbuzi hili tatizo” alisema Basilu
Mwenyekiti wa kijiji
alilipongeza shirika la LEAT kwa kutoa elimu iliyowafumbua macho wananchi wa
kijiji cha Ihefu na ndio kitu ambacho miaka minigi tulikuwa tunatakiwa
kukifanya kwa wananchi wawe na uelewa wa maliasili zao pamoja na kujua kila mpango
wa maendeleo ya kijiji.
Naye mtendaji wa kijiji
Paulo Magala alikili kutoitisha mkutano wa mapato na matumizi kutokana na wananchi
kutoitikia wito wa kufika kwenye mkutano ili wasomewe mapato na matumizi.
Akijibia tuhuma juu ya
upotevu wa shilingi milioni ishirini na tano alisema kuwa hakuna upotevu wa
pesa hizo na kuambia wananchi wawasubili wanasheria wa wilaya ndio watakuja na
majibu yote kwa kuwa amejipanga na anavielezo vyote ambavyo vinaonye matumizi
ya hizo fedha.
Magala aliongeza kuwa
wananchi wamekuwa na uelewa kutoka na kupewa elimu na shirika la LEAT kutoa
elimu ya uwazi na uwajibikaji kitu kinachotufanya wananchi wewe wanahoji kila
muda na kutufanya viongozi kila muda kujibia kero za wananchi a sio kupanga
mipango ya wananchi
0 comments:
Post a Comment