Saturday, April 8, 2017

RITTA KABATI AANZA KUKARABATI SHULE YA MSINGI KIGONZILE

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikabidhiwa msaada wa mifuko ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Kigonzile na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la bima (NIC)  Tanzania Samwel Kamanga
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la bima (NIC)  Tanzania Samwel Kamanga akimkakabidhi kiasi cha Pesa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati zilizochangwa na baadhi ya wadau walijitokeza kwenye ukarabati wa shule ya msingi Kigonzile
Baada ya kufanikiwa kukarabati shule ya msingi Azimio iliyopo Kata ya Mshindo Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ameanza kukabati shule ya msingi Kigonzile iliyopo Kata ya Nduli kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwapo shirika la bima Tanzania (NIC)ambao walijitokeza kusaidia ukarabati wa shule hiyo ya Kigonzile.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vitakavyo tumika katika kukarabati shule hiyo Kabati alisema kuwa amuamua kufanya shughuri za kijamii ili kuifanya jamii ya watu wa Iringa kuwa na Elimu iliyobora na kuweza kuwa na kizazi ambacho kitakuwa cha kimaendeleo.

"Mimi sipendi kuona watoto wa Iringa wanakuwa wafanyakazi wa kazi za ndani kwa watu kwenye Pesa au wafanyakazi wengi najiuliza tu kwanini ile Iringa ndio chimbuko la wafanyakazi wa kazi za ndani,nitapambana kuhakikisha Iringa inakuwa na wasomi wengi ili kupunguza utegemezi"alisema kabati

Kabati alisema kuwa kuna shule nyingi zimehalibika hapa Manispaa ya Iringa hivyonitakikisha natafuta wafadhili mbalimbali kila kona hapa nchini na nje ya nchi ili kuhakikisha tunazikarabati shule zote ambazo chakavu.

"Hii ni moja ya shule ambazo tayari nimeanza kuitafutia wafadhili hivyo hata shule nyingine nitahakikiaha nafanya kazi na serikali yangu ya chama cha mapinduzi (CCM) chini ya Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuli ambaye anaongoza vizuri sana " alisema Kabati

Aidha Kabati aliomba wananchi kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi kuleta maendeleo kwa kuwa wakiitegemeea serikali tu hawawezi kupiga hatua ya kimaendeleo kutoka hapa walipo na kuweza kufikia malengo ya juu kimaisha.

Lakini Kabati aliwaomba viongozi na serikali kutafuta wahisani mbalimbali kila mahali ili kuweza kufanikisha kufikia malengo ya kimaendeleo na kuacha kuwa tegemezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la bima (NIC)  Tanzania Samwel Kamanga alisema kuwa ameguswa sana na uchakavu wa shule ya msingi Kigonzile kwa hali iliyonayo hivyo licha ya kuwa amechangi zaidi ya 160 ya mifuko ya saruji kwa ajili ya ukarabati.

"Mimi nimesoma kwenye shule kama hii na ndio sababu Leo hii nipo hapa kama Mkurugenzi hivyo Leo nimeguswa sana hii shule imeharibiaka sana na inahitaji Pesa nyingi hivyo tumetoa kiasi kidogo sana narudi makao makuu ya shirika letu nitatoa jibu kwa namna gani nitasaidia kuiboresha na kuwa kama shule nyingine za watu binafsi"alisema Kamanga

Aidha Kamanga aliwaomba wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya taifa ili kuepukana na kupunguza gharama wakati wa majanga kwa kuwa hujui lini utakumbana na matatizo ni vyema wananchi wakajua umuhimu wa bima ya afya ya taifa inamsaidia kimaisha.

Nae Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alimshukuru mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuleta maendeleo katika Mkoa wa iringa kwa kufanya kazi nyingi za kijamii tofauti na wanasiasa wengine.

"Tukiwa na wabunge kama Hawa basi nchi itapiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwa kuwa watakuwa wachapakazi na sio waroho wa madaraka wala sio wapenda Pesa basi tutatoka hapa tulipo na kufika kule tunako staili" alisema Kasesela

Ila Kasesela aliwaomba viongozi wa serikali na wananchi kutumia bima ya taifa ya Tanzania NIC kwa kuwa imekuwa inafanya kazi zake vizuri kuliko bima nyingine hivyo ni lazama kuitambua bima hiyo kwa kuwa ni ya uhakika tofauti na bima nyingine zilizopo hapa nchini.

Nao baadhi ya wananchi wa Kata ya nduli mtaa wa Kigonzile waliwashuku viongozi wa serikali, shirika la bima ya taifa,diwani pamoja na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati kwa Juhudi kubwa za kukarabati shule hiyo ya Kigonzile kwa kuwa ilikuwa katika wakati mgumu sana.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More