NA MZIDALFA ZAID(ARUSHA)
Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti na tukio la kwanza ni kifo cha kinyama cha mtu mmoja kukatwa shingo yake na kitu chenye ncha kali huku mtu mmoja akifariki dunia kwa kupatwa na mshituko wa moyo baada ya kwenda shambani mwake na kukuta majani yamezidi mazao hapa wilayani babati mkoani manyara.
Katika tukio la kwanza mtu huyo alieuwawa mithili ya nguruwe kwa kukatwa shingo yake kwa panga na kuchomwa kisu kikali mdomoni mwake katika kijiji cha majengo kilichopo kata ya kashi wilayani babati mkoani manyara ambapo ametambulika kwa majina ya hamis hasan nyalu.
diwani wa kata hio ya kashi John kanda amethibitisha mtu huyo kuwawa ambaye ni mkazi wa eneo lake na alikua akiishi mpakani mwa mkoa wa manyara na dodoma majengo.
Kamanda wa polisi mkoani manyara kamanda francis masawe amesema kua tayari maafisa wa jeshi la polis wamekwishafika fika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehem huyo na kuupeleka katika zahanati ya galapo wilayani babati mkoani hapa kwa uchunguzi.
0 comments:
Post a Comment