NA MZIDALFA ZAI(ARUSHA)
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kwa
kushirikiana na Wakili wa Serikali wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora imewapandisha
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Igunga viongozi
watatu wa serikali ya Kijiji cha Isenegeja kwa tuhuma za wizi wa fedha za
serikali.
Waliopandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo ni pamoja na
Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Isenegeja,Ahmed Jambeck(50),Mjumbe wa
serikali ya Kijiji cha Isenegeja,Seleli Kashindye (58) na aliyekuwa Kaimu afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Isenegeja Michael John (47) wote wakazi wa kijiji hicho.
Awali Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU)kutoka Mkoani Tabora,Edson Mapalala wakishirikiana na
wakili wa serikali kutoka Mkoani Tabora,Tumaini Pius alida kuwa washitakiwa
wote watatu wanashitakiwa kwa makosaa mawili likiwemo la wizi wakiwa watumishi
wa serikali ya Kijiji cha Isenegeje huku shitaka la pili likiwa ni wizi.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo,Ajali Milanzi,Mwendesha Mashataka
huyo alidai kwamba washitakiwa hao walitenda kosa hilo kati ya mwaka 2008 na
2015 wakati wakiwa watumishi katika Kijiji cha Isenegeja kwa pamoja waliiba
shilingi 34,131,000/= mali ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo Mapalala alidai Mahakamani hapo kuwa baada ya
washitakiwa hao kufanya wizi huo,walibadilisha matumizi yao binafsi ya fedha
hizo bila kuwa na kibali cha kufanya hivyo.
Aidha Mwendesha Mashitaka alidai Mahakamani pia kwamba washitakiwa
walitenda kosa la kwanza kinyume na kifungu 271 cha kanuni ya adhabu sura 16
mapitio ya 2002 na kosa la pili walitenda kinyume na kifungu 258, 1, 265 cha
sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002.
Hata hivyo baada ya kusomewa mashita hayo mawili,washitakiwa wote
watatu wamekana kutenda makosa hayo na kwamba wote wapo nje kwa dhamana ya
shilingi milioni 35 kila mmoja hadi Apr,19,wmwaka huu kesi hiyo itakpotajwa tena.
0 comments:
Post a Comment