Awali, Kiwanda cha Karanga kilichopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kilishindwa kuendelezwa.
Ili
kufanikisha hilo, tayari Shule ya Sekondari ya Bwawani inayomilikiwa na
jeshi hilo imeanzisha mtalaa wa masomo ya sayansi ili kuandaa vijana wa
kufanya kazi viwandani.
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza, Gaston Sanga alisema mikakati hiyo inalenga kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kutilia mkazo ukuaji wa uchumi kupitia viwanda.
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza, Gaston Sanga alisema mikakati hiyo inalenga kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kutilia mkazo ukuaji wa uchumi kupitia viwanda.
Alisema taaluma inayotolewa shuleni hapo itakwenda sambamba na mahitaji ya wataalamu watakaotumika katika viwanda hivyo.
“Tumeona
tuanzishe mchepuo wa masomo ya Sayansi yaani CBG (Kemia, Bailojia na
Jiografia) kuanzia mwakani katika shule yetu ya Bwawani,” alisema kamishna huyo.
Alifafanua
kuwa wameanzisha masomo hayo ili kupata wataalamu wengi watakaovisaidia
viwanda vya jeshi na vingine vilivyopo nchini.
Kamishna
Sanga alisema katika kuimarisha na kujenga upya kiwanda cha viatu na
kile cha sukari, wanashirikiana na mifuko ya hifadhi za jamii ya PPF na
NSSF.
Kuhusu
Shule ya Sekondari ya Bwawani, alisema maendeleo ya kitaaluma
yanategemea miundombinu ya madarasa, maabara, maktaba na ubora wa afya
ya mwanafunzi.
Alipongeza
jitihada zinazofanywa za kukamilisha kuendeleza miradi mbalimbali
katika shule hiyo ili kuboresha maendeleo ya kitaaluma.
Pia,
alisema ni vyema wazazi wawe mstari wa mbele kulipa ada kwa wakati ili
kuwaruhusu wanafunzi kurudi shule mapema na walimu waweze kwenda
sambamba na mitalaa iliyopo.
Kamishna
Msaidizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga ambaye pia ni mkuu wa sekondari
ya Bwawani, alisema pamoja na jitihada za ujenzi wa nyumba mbili za
walimu kwa mfumo wa kujitolea na madarasa mawili, bado wanakabiliwa na
changamoto ya ukosefu wa jengo la utawala na nyumba za watumishi.
0 comments:
Post a Comment