Monday, April 10, 2017

MBUNGE BUPE MWAKANG'ATA AIPIGA TAFU SHULE YA MSINGI KIGOZILE

 Mbunge viti maalumu mkoa wa rukwa Bupe Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji
 Mbunge viti maalumu mkoa wa rukwa Bupe Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi kiasi cha shilingi laki mbili kwa ajili ya kuongezea kununua mifuko ya saruji kwa ajili ya kukarabati shule ya kigonzile

Na Fredy Mgunda,Iringa
Mbunge viti maalumu mkoa wa rukwa Bupe Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) ameipiga jeki shule ya msingi Kigonzile iliyopo kata ya Nduli mkoani iringa kwa kuipatia mifuko zaidi ya ishirini ya saruji kwa lengo la kusaidia ukarabati wa shule hiyo akiwa na lengo la kumuunga mkono mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati katika juhudi za kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi saruji hiyo Mwakang'ata alisema kuwa ameamua kumuunga mkono mbunge huyo kwa kuwa ni mpenda maendeleo na mchapa kazi.

“Mimi napenda kufanya kazi za kimaendeleo hasa za kijamii ndio maana kabati aliponiambia kuwa anakuja kufanya maendeleo ya ukarabati wa shule ya msingi kigozile nilikubali haraka kwa kuwa na napenda kufanya maendeleo” alisema Mwakang'ata

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli  ametutuma kufanya kazi kwa wananchi wakawaida kwa kuwa wao ndio wanamahitaji mengi kuliko watu wa kipato cha kati na cha juu hivyo hata mimi nimeamua kufanya kazi za kwasaidia kuleta maendeleo wananchi wengi wa chini.

Aidha Mwakang'ata aliwaomba wananchi na viongozi wa kufanya kazi kwa kujituma ili kwenda sambamba na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Magufuli na kuomba jamii kufanya kazi za kujitolea zaidi kuliko kusubili serikali kuleta maendeleo.

“Mkiwa mnajitolea kama hii leo naamini tukiwa na wananchi na viongozi wengi basi nchi hii itapata maendeleo ya haraka na kwa kasi kutokana na wananchi kufanya kazi kwa nguvu na moyo wa kuinua uchumi” alisema  Mwakang'ata

Mwakang'ata aliongeza kuwa shule nyingi za hapa nchi zilijengwa miaka mingi iliyopita hivyo nyingi zimechakaa kutokana na kutokarabatiwa kwa wakati hivyo nawaomba viongozi wengi kuwa wabunifu wakati wa kutafuta pesa nyingi za kusaidia kukarabati miundombinu ya shule na maeneo mbalimbali ilimradi kukuza uchumi na kutoa elimu bora.

“Hichi nilichokitoa hii leo ni kidogo sana ila nimefurahishwa na kujituma kwenu katika swala nzima la kusaidia ukarabati wa shule hii ya kigonzile ambayo ilikuwa katika mazingira ya kufungwa kutokana na uchakavu wake” alisema Mwakang'ata

Mwakang'ata namkaribisha pia mbunge Ritta kabati kuja Rukwa pia aje asaidie maendeleo kwa kuwa naye ni mpenda maendeleo na wananchi wa Rukwa wanapenda maendeleo na ninahakika watampokea kutokana na uchapakazi wake.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More