Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu, Raymond mwangwala Amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya ukerewe.
Leo katibu wa ccm mkoa wa mwanza akiambatana na kaimu katibu uvccm mkoa wa mwanza ndugu Benedikto Bujiku na kaimu katibu wa UWT mkoa wa mwanza pamoja na muenezi wa CCM Mkoa wa mwanza, wamefanya ziara katika wilaya ya ukerewe kwa kukutana na wajumbe wa kamati ya siasa pamoja na sekeretalieti ya ccm wilaya ya ukerewe.
Pamoja na mambo mengine katibu wa ccm mkoa wa mwanza amepokea changamoto mbalimbali zilizoko katika wilaya ya ukerewe na kuhaidi kuzitatua kwa wakati .
Pia katibu amewataka viongozi wa chama na jumuiya kuendelea kufatilia muenendo wa utoaji fomu za uchaguzi za matawi na mashina ili kufanikisha zoezi ili vizuri.
Lakini pia katibu amewataka viongozi wa chama kuhakikisha katika uchaguzi huu ndani ya chama vitendo vya Rushwa vinapigwa marufuku .
Katibu pia amewataka watendaji wa chama kuwa waaminifu na wafanye kazi kwa weledi mkubwa ili kufanikisha chaguzi ndani ya chama, Katibu alisema kuwa mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa maandalizi ya chaguzi zingine kwahiyo tukiharibu sasa hivi tujue kabisa tunaharibu uko tuendako katika chaguzi za na serikali.
Katibu aliupongeza umoja wa vijana wa ccm kwa namna ambavyo wanajitaidi kujibu hoja za wapinzani mitandaoni lakini pia aliupongeza kwa namna ambavyo wanajitaidi kufanya kazi vizuri katika maeneo mbali mbali katika wilaya hiyo, pia katibu alizidi kukipongeza chama kwa namna ambavyo kimeshusha maelekezo ya uchaguzi kwenye matawi na kata. Katibu amemaliza ziara yake na kurudi mjini mwanza.
Binafsi tunawashukuru saana viongozi wa chama ngazi ya mkoa kwa kushuka uku chini kuangalia muenendo za chaguzi ndani ya chama.
0 comments:
Post a Comment